Dalili za magonjwa ya akili

Dalili za magonjwa ya akili

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Dalili zinazoashiria magonjwa ya akili ni nyingi sana, baadhi tu ni ambazo zimegawanyika katika makundi matatu ni kama ifuatavyo:

i) Kihisia

· Kukosa furaha na kuhuzunika sana

· Kuwa na furaha sana kupita kiasi

· Wasiwasi na/ au woga kupita kiasi

· Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi

· Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine

· Kuwa na msongo wa mawazo

· Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida

· Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha

· Kutokuonyesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk)

· Kutokujijali usafi na muonekano wake

· Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.

ii) Kimwili

· Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi

· Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi

· Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula

· Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza

· Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.

iii) Kiakili

· Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku

· Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu

· Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti

· Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo

· Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake ; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni Nabii
au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu

· Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili yake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza

· Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinazungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye

· Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.
 
vizuri ila umeyatoa wapi mbona kama ni ivyo kila mtu ni mgonjwa wa akili basi
 
mwe! mbona hivyo tena maana hizo dalili nyingi kweli ina maana tuliowengi tutakuwa vichaa!!!!!
 
Inabidi Majengo ya Milembe Dodoma yaongezwe.... Maana hizo dalili ni hatari sanaa!![emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Dalili zinazoashiria magonjwa ya akili ni nyingi sana, baadhi tu ni ambazo zimegawanyika katika makundi matatu ni kama ifuatavyo:

i) Kihisia

· Kukosa furaha na kuhuzunika sana

· Kuwa na furaha sana kupita kiasi

· Wasiwasi na/ au woga kupita kiasi

· Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi

· Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine

· Kuwa na msongo wa mawazo

· Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida

· Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha

· Kutokuonyesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk)

· Kutokujijali usafi na muonekano wake

· Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.

ii) Kimwili

· Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi

· Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi

· Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula

· Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza

· Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.

iii) Kiakili

· Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku

· Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu

· Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti

· Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo

· Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake ; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni Nabii
au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu

· Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili yake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza

· Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinazungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye

· Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.

Sikubishii na ni kweli karibu wote ni " mitambo " ila naomba kuuliza vipi na huyo au hao waliyoyagundua haya? Kwani nahisi wao ndiyo watakuwa na matatizo ya akili tena ya kutukuka kabisa.
 
Kupiga puli zaidi ya mara moja kwa siku
 
hapo naona umechambua kiundan zaid kauli ya binadam wote n vichaa sema kila mtu ana level yake ya ukichaa
 
Sikubishii na ni kweli karibu wote ni " mitambo " ila naomba kuuliza vipi na huyo au hao waliyoyagundua haya? Kwani nahisi wao ndiyo watakuwa na matatizo ya akili tena ya kutukuka kabisa.
Imetoka kwa madaktari wa magonjwa wa akili...wana uzoefu na magonjwa hayo
 
Back
Top Bottom