Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Unyanyasaji wa Mtandaoni, unazidi kuwa tishio kubwa kwa watoto kila mahali duniani. Dalili zake mara nyingi hazionekani moja kwa moja, lakini zinaweza kufahamika iwapo kirahisi kama tu mzazi au mlezi utaweka umakini kwa mwanao.
Mtoto aliyeathirika anaweza kuonekana mnyonge au mwenye huzuni kila anapotumia mitandao.
Mara nyingi hujitenga na wenzake, anaweza kuonesha mabadiliko ya kimwili kama kupungua uzito au mabadiliko yasiyo ya kawaida ya kimwili au hisia zake.
Pia, unaweza kugundua kama mtoto amekuwa msiri kuhusu anachofanya mtandaoni, au ameanza kuwasiliana na watu wapya bila maelekezo ya wazazi
Muda wa matumizi ya Simu au vifaa vya kidijitali unaongezeka, na mara nyingine, mtoto huchelewa kurudi nyumbani bila sababu za kueleweka.
Ni jukumu la kila mzazi au mlezi kuwa makini na dalili hizi. Chukua hatua mapema kumlinda mtoto wako dhidi ya madhara ya unyanyasaji wa mtandaoni.