Dalili za mume anayetembea na "house girl"

Ba mdogo wangu mchezo wake mkubwa ni pamoja na kutembea na mabaa maidi na mahausi geli wake!
 
Ahsante saana kwa ushauri wako kwa wanaume na wanawake wenye tamaa za mbwa. Watu wanatakiwa wajiheshimu kwenye majumba yao, kuanzia mama mwenye nyumba, baba, watoto hadi watumishi. Njia rahisi ya kuweka mji wako vizuri ni kuupeleka mbele za Mungu, yeye ndiye mlinzi hodari kabisa. Kila wakati wewe na mkeo peleka nyumba yenu mbele za Mungu kwa maombi, maana mji ni mwanzo wa kulijenga taifa. Mungu asipolinda nyumba yako hata ukikesha unafanya kazi bure. Ubarikiwe mleta mada!!!!!!!!!
 
DALILI YA TATU (SI KWA HAOUSEGIRL TU, KWA UJUMLA NI DALILI ZA MWANAUME ANAYETOKA NJE YA NDOA YAKE)
Mwanaume utamuona ana-pretend kuonya upendo saaana kwa mkewe kuliko siku zote, tena atajifanya kuleta zawadi mbalimbali ambazo si kawaida yake, na kama ana uwezo hata gari anaweza kukununulia au zawadi yoyote ambayo wewe kama mkewe utaona si kawaida, na kama alikuwa mkali anapunguza, anajichekesha chekesha ili mradi usigumndue kinachoendelea!!!! Hii nimwshaona live kwa mama mmoja ambaye alikuwa ana ugomvi almost kila siku na mumewe. Ghafla mume akabadilika, akawa anampenda mkewe ukiwaona hadi raha!! asemacho anapewa, zawadi za hapa na pale ndo usiseme, kumbe anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!!!!
 
Boara hata ungeandika sababu za mume kufikia hatua ya kumnyatia house girl!!mambo yote hayo umeyajuaje??kama hujapitia huko?wewe inaonekana unaweza kuwa hata mwizi wa pesa maana unambinu kama Osama!
 
mim sijambo hofu kwako uliyenitelekeza,
yep,sisi no housegirl,
ni houseboy tu
Mi mzima,si tilielewana tutasaidiana kazi ? hili la hausiboi limetoka wapi ? kama hivo inabidi hausigeli nae awepo ili kunipashia chakula na kuanda ustaarabu wa kuoga nikichelewa kurudi lol! na siku moja moja kunipa kampani kuangalia TV ukilala mapema sawa ?
 

yaani mara hii umeshasahau kuwa tulisema tusiruhusu kabisa housegirl ktk nyumba yetu?
mi naomba dear tusibadili huo uamuzi,sitaki housegirl,
hapo red naona ka unanitusi,hayo yote mbona nakufanyia au kuna siku nililalamika?
ni kweli uliniahidi kunisaidia kazi lkn siku hizi hunisaidii uko busy sana na rafiki zako,
ucjal nitaenda mwenyewe kijijin kwetu kutafuta kijana mtiifu aje anisaidie kaz,

najua umeshakubali,si unajua kitu kimojawapo nilikupendea wewe sio mbishi.
 

True afrodenzi, 'it's just a matter of time' nisingependa kuwa na mtu asiyeniamini wala siwezi pata muda wa kufuatilia mtu mzima.
 
Naona umepania kuleta hausiboi sasa nakubali umlete nami namleta kuna hausigeli kutoka Singida mtaa wa pili naona atatufaa.
 
Mi naombeni part 2 ya hii muvi,,

"Dalili ya mke anayetembea na houseboy"
 
Hivi huyo aliyeandika hayo yamemkuta au nae yumo? anaonesha ni mtaalam wa haya masuala.
 
Wrong strategy. Dawa ya mchawi mpe mtoto alee mwenyewe. Na dawa ya mme/ke mkware mkabidhi housegirl/boy na usipoteze muda kuwafuatilia. Kumbuka unavyozidi kubana ndio hamu ya mhusika ya kutafuta upenyo wa kutenda inazidi.
 
Naona umepania kuleta hausiboi sasa nakubali umlete nami namleta kuna hausigeli kutoka Singida mtaa wa pili naona atatufaa.

nilikua nakutania tu,ahirisha kabisa hiyo mipango,mim ndo housegirl na mim ndo housewoman but not housewife.
 

olewa na mzungu mwaya,wanacheat ila sio kama waafrica,waafrica kuwa na nyumba ndogo ni kama utamaduni lol,eti ndio uanaume?!
 
Part two of the story:

Mume kama ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wa kazi, ikitokea mke amesafiri ni nafasi kubwa sana kwao kujiachia.

Ni katika kipindi hicho, hausigeli ataweza kuingizwa hadi chumbani na kulala. Tena wengine hujiachia vibaya, kwani hata akiamka asubuhi anaweza kuacha khanga yake ikiwa imeandikwa; Paka Akitoka Panya Hutawala.

Sasa mke utaijuaje tabia hii? Ni rahisi sana, ukiwa safarini utashangaa ukimpigia simu mumeo saa kumi na mbili jioni na kumuuliza aliko atakujibu nyumbani wakati kawaida yake hurudi saa nne mpaka tano usiku.

Asubuhi, kama kawaida yake kwenda kazini ni saa moja utashangaa kumsikia mpaka saa mbili kasoro hajaondoka na sababu anazokupa hazina maana.
Wakati mwingine pia, ukimpigia simu usiku atachelewa kupokea au akipokea maongezi yake yanaashiria kutaka mmalize haraka. Ni kwa sababu yupo na msichana wa kazi pembeni.

Mapenzi ya aina hii yakifikia hapa, mke ndani ya nyumba anakuwa anaishi katika hatari kubwa ya talaka au ugomvi wa mara kwa mara. Na kama msichana huyo wa kazi amejaaliwa uzuri, hakika ndoa hupinduka na yeye kuchukua nafasi.

Wapo wanawake kibao mitaani ambao ndoa zao zilipinduliwa na wasichana wa kazi. Hufika mahali akitaka kwenda kuwaona watoto anakuwa mwizi, anafikia nyumba ya jirani na kuwaita.
Nakupa mfano mmoja; huu ulitokea wilayani Korogwe, Tanga. Dada mmoja (jina ninalo) aliolewa na kubahatika kuzaa watoto wawili wa kiume.

Lakini alichokosea ndani ya nyumba yake, alimwachia msichana wa kazi kuendesha kila kitu. Mume akirudi anakumbana na huduma kutoka kwa dada, asubuhi akitaka kwenda kazini anakumbana na huduma za hausigeli, mwishowe wakajenga uhusiano wa kimapenzi.

Imekwenda, mke hajui, ikafika mahali mume akamrudisha mke kwao kwa kisa kidogo tu, alimjibu jeuri. Akiwa nyumbani kwao, mke akapata habari kwamba, mumewe amefunga ndoa na msichana wa kazi tena akiwa mjamzito.

Ikawa mke huyo akienda kuwaona watoto wake anakaribishwa na msichana wake wa kazi, anamuandalia chumba cha kulala ambacho awali alikuwa akilala yeye. Mama akawa hana chake.
Haya yote ni madhara ya kuwaachia wasichana wa kazi wafanye kila kitu kwa waume ndani ya nyumba. Ni hatari kuliko inavyofikiriwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…