Kila Malaika alipewa kazi yake na Mwenyezi Mungu ..na sio kwamba Mungu hana uwezo wa kufanya hizo kazi peke yake maana yeye ni muweza wa yote na hakuna linalomshinda.
Yeye akisema kuwa basi kitu kinakuwa, sasa basi, aliwapa Malaika kazi za kufanya kwasababu ya kuonesha kwamba hana ubaguzi na viumbe wake.
Na ndio Malaika wakajisikia faraja kuachiwa kazi mbali mbali wafanye wao kwa amri ya Mungu.
Ngoja niwaweke majina ya Malaika wakubwa na kazi zao.
1. RIDHWAAN: Huyu alipewa kazi kulinda milango ya peponi.
2. MAALIK: Kazi yake kulinda milango ya motoni.
3. ISRAFIIL: Huyu alipewa kazi ya kuja kupuuliza parapanda siku ya kufufuliwa (kiama).
4. MIKAIIL: Alipewa kazi ya kuruhusu mvua kunyesha pamoja na mimea.
5. ZIRAIIL: Kazi kusubiri amri kwa Mungu nane anamuhitaji yeye anaenda kuifanya kama walivopewa majukumu wengine. Kwahiyo sasa ..kila mtu anamjua huyo Malaika kwakuwa kapewa jukumu zito linalogusa nyoyo zetu, kwa leo niishie hapo.