Dalili za Rushwa: Magari binafsi ya Traffic yanapotumika kukamata magari

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Ni kawaida siku hizi kuona askari wa usalama barabarani wakiwa na magari yao wemeyaweka vichakani wakisimamia sheria za barabarani au wakifanya kazi ya kukamatakamata.

Magari haya unaweza kuyakuta mbali tena yakiwa nje ya mji.

Swali la kujiuliza. Nani anaweka mafuta haya magari kuyawezesha kuwa maeneo hayo.

Uhalisia ni kwamba, askari hawa huweka mafuta na hawana namna ya kupata pesa zao zaidi ya kutoka kwa watumia barabarani.

Kwa lugha rahisi, rushwa za barabarani zitapungua pale vitendea kazi vitakapokuwa vya kutosha.

Vinginevyo, tutalipia sana mafuta ya askari na ndio rushwa husika.
 
Labda sheria ya polisi trafiki inawaruhusu wafanye hivyo. Umeuliza swali la msingi sana nani anawawekea mafuta. Mfano pale Mapinga ama pale njia ya kwenda Mbegani na kabla ya kuingia Bagamoyo kuna sehemu kuna mwembe wanapaki gari zao binafsi.

Ni wezi mtupu. Trafiki ni kirusi hatari zaidi ya kansa kwa kubobea kwenye rushwa hawa walitakiwa wote watolewe wakalinde vitasa.
 
Hii imekuwa hulka. Wapo maeneo yote. Wengine wanafanya doria na gari zao usiku.
 
Wajinga sana wanatabia ya kukimbiza magari kwa bodaboda hawa hawana maadili kbs ya kazi. Hakuna trafiki ambaye atanikamata awe na gari lake nitamvunjia vioo hatoamini..wapo hapa Bucha Kimara na rombo asubuhi wanataki magari yao barabarani kabisa kusudi ukanyage lane ya mwendokasi wakulipishe.
 
Hilo mm linanishangaza sana "askari anatumia Racts au IST au alphad kukamata magari ya watu binafsi
 
Wajinga sana wanatabia ya kukimbiza magari kwa bodaboda hawa hawana maadili kbs ya kazi. Hakuna trafiki ambaye atanikamata awe na gari lake nitamvunjia vioo hatoamini..wapo hapa Bucha Kimara na rombo asubuhi wanataki magari yao barabarani kabisa kusudi ukanyage lane ya mwendokasi wakulipishe.
ukivunja kioo utalipa,hata kwa makofi.
 
Kati ya wew unaeombwa Rushwa na hao Traffic bila kuwareport,

Na hao Traffic wanaokuomba Rushwa nani ni Kirusi Mkuu
 
Nachojua magari mengi ya PT serikali ndio inagharamikia mafuta
Wadau ndio tunaojaza mafuta ktk magari ya polisi.Nasikia wakisema mara nyingi eti bajeti yao ni ndogo.
Serikali itazame hili huenda ikawa ni kweli,kitendo cha polisi kuomba msaada wa mafuta kwetu sisi matajiri inadhohofisha utendaji kazi wao.
 
Kati ya wew unaeombwa Rushwa na hao Traffic bila kuwareport,

Na hao Traffic wanaokuomba Rushwa nani ni Kirusi Mkuu
mtu anaombwa rushwa badala akomae kulipa fine 30,anatoa rushwa 2k halafu anakuja kulia lia huku!!!

unafiki.
 
Ni kawaida siku hizi kuona askari wa usalama barabarani wakiwa na magari yao wemeyaweka vichakani wakisimamia sheria za barabarani au wakifanya kazi ya kukamatakamata.
Magari haya unaweza kuyakuta mbali tena yakiwa nje ya mji.
Swali la kujiuliza. Nani anaweka mafuta haya magari kuyawezesha kuwa maeneo hayo.
Uhalisia ni kwamba, askari hawa huweka mafuta na hawana namna ya kupata pesa zao zaidi ya kutoka kwa watumia barabarani.
Kwa lugha rahisi, rushwa za barabarani zitapungua pale vitendea kazi vitakapokuwa vya kutosha.
Vinginevyo, tutalipia sana mafuta ya askari na ndio rushwa husika.
Inafikirisha sana
 
Gari inakua on muda ,anapigwa na ac ndani kama yupo ofisini ,vioo vimefugwa asionekane .matumizi mabaya ya Pesa zetu,bora warudi kupanda juu ya miti na kujificha maporini wapambane na nyoka uko
 
mtu anaombwa rushwa badala akomae kulipa fine 30,anatoa rushwa 2k halafu anakuja kulia lia huku!!!

unafiki.
Huu mjadala ni wa kimfumo. Sio wa mtu kutoa 2k. Tunaangalia vichochezi vya rushwa jinsi vilivyo wazi.
Tungefika kwenye camera au matumizi ya teknolojia, tatizo hili lingepungua sana.
 
rushwa ni maamuzi na tabia,ni ngumu kupigana na rushwa kama mtoaji anafanya unafiki.
 
Magari binafsi yanatumika

Au ni polisi kaenda alipopangiwa kazi kwa kutumia usafiri wake????
 
Back
Top Bottom