Dalili za Rushwa: Magari binafsi ya Traffic yanapotumika kukamata magari

rushwa ni maamuzi na tabia,ni ngumu kupigana na rushwa kama mtoaji anafanya unafiki.
Pamoja na mtoaji, huyu mpokeaji anayetumia usafiri wake binafsi kwenda kusimamia sheria. Matokeo yake ni kulipwa pesa binafsi ambayo ndiyo rushwa.
 
Pamoja na mtoaji, huyu mpokeaji anayetumia usafiri wake binafsi kwenda kusimamia sheria. Matokeo yake ni kulipwa pesa binafsi ambayo ndiyo rushwa.
jukumu lako ni kudai risiti ya kodi halali.

sio unampa buku mbili halafu unakuja kutafuta ufumbuzi huku,ni ujinga.
 
jukumu lako ni kudai risiti ya kodi halali.

sio unampa buku mbili halafu unakuja kutafuta ufumbuzi huku,ni ujinga.
Usihangaike na utetezi, tutengeneze mfumo unaootoa haki. Kupokea buku 2 na kutoa yote ni matatizo.
 
Na humo ndiyo hukusanyia rushwa, mfano halisi na hai ni traffic police wanaojificha kwenye kile kichaka cha opposite na shule ya msingi Sokoine Mvomero na wale wa Sido Iringa
 
Trafik bhana unakuta gari wanayotumia wao waliyoipaki pembeni ni chakavu balaa harafu wao wanakagua ya wengine wajivunje kwa madiba gari za metro au polisi hazina chenga hata kidogo gari za jamaa zetu zingine hata kujua tuu ni rangi gani ni mtihani sijui zinapakwa za nyumba zile...
 
Swadakta!
 
Hii ya kutumia magari binafsi ilipungua baada ya kelele za jukwaani.
Dalili ni kwamba, hawa watu wameanza tena hivyo kuhalalisha kujaziwa mafuta kwa rushwa lakini hata askari wasio waaminifu kujitokeza barabarani huku wakiwa kwenye siku za mapumziko.
 
Niliwahi mara kadhaa kupita Barabara ya arusha-kisongo , kila hiace ya abiria ikifika pale tawi la shule ya Moshi international/mkabala na gereza la kisongo kondakta au dereva hushuka na kukabidhi kwa trafic 2000/-.hakuna ukaguzi au kazi nyingine hapo zaidi ya kupokea hizo 2000/- kundi lingine la matrafic utalikuta barabara ya kuingia mahakama ya ruanda(haki road).rushwa ni donda ndugu hakika. Toa 2000/- au gari likaguliwe uandikiwe kosa na faini ya 30,000/- kazi ni kwako !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…