Dalili za ugonjwa mpya wa ukosefu wa pesa

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,875
Habari wakuu!

Baada ya kufanya uchunguzi wangu toka mwaka huu uanze juu ya dalili kadhaa za ndugu zangu, majirani zangu, wafanya kazi wenzangu na hata mimi mwenyewe kwa nyakati tofauti nimegundua kwamba kuna ugonjwa mbaya sana wa ukosefu wa pesa miongoni mwa watanzania. Ugonjwa huu huambatana na dalili kadhaa ambazo ni hatari kuliko hata zile za malaria. Dalili zenyewe ni kama zifuatazo:
-Hasira za karibu
-Kulaumu watu wengine kwa mambo madogo madogo sana
-Wivu kwa wengine wenye hali nzuri kidogo
-uchoyo wa kutotaka hata wageni
-Kuogopa kupigia ndugu simu kwa hofu ya kuombwa hela
-Kuogopa kupokea simu za ndg, jamaa na marafiki
-Kulialia maisha ni magumu hata kabla hujaulizwa
-Kuchapa na kukoromea watoto au mwanamke kwa makosa madogo madogo
-Kutokupenda vyakula vya mafuta mafuta kwa lengo la kupunguza mwili
-Kichwa kuuma kutokana na mawazo
-Mwili kuchoka na kushindwa kupata usingizi
-Kugombana na makonda na abiria kwenye magari ya umma

Kama unapata dalili tajwa hapo juu au baadhi za dalili hizo unazo basi wahi mtwara msimu huu kuna kazi ya kubangua korosho. Dalili zikizidi kachukue fomu za chadema kisha baada ya wiki au mwezi ita waandishi wa habari kisha mwaga matusi kwa mabosi wako hasa bosi mkubwa, dai umetishwa kwa kuulizia ruzuku na kutaka kugombea nafasi yake kisha jiunge kule kwingine na mwaga sifa zote kwa baba mwenye nyumba huenda ukabahatika kupunguza makali ya maisha.

Pamoja na ugonjwa huu mbaya kuna ugonjwa unaoibuka kwa kasi sana karibia na mwisho wa mwezi. Ugonjwa huu ndiyo utakaotoa roho za watu wengi maana huambatana na kuongea mwenyewe njiani na kuchorachora hewani kwa mkono kama mtu anayefanya mahesabu ya complex numbers. Kuvurugwa na kutamani kujinyonga, kutamani kuacha kazi na kurudi kijijini kwa wingi wa lawama za ndugu na wazazi, kushindwa kujua nini cha kufanya na kubaki kama mtu mwenye mtindio wa ubongo kunakosababishwa na kuisha kwa pesa kabla ya kuzipokea mkononi.
Kama unajua dalili nyingine za magonjwa haya plz weka hapa tuyaone.

Kindi -Tandahimba
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
1.Kuulizia chenchi kwa ukali hata kama imebaki Sh 100 baada ya kununua kitu.
2.Kuisi umelogwa huku aliyekuroga humjui
3.Dominant mboga kwenye familia ni maharage
 
Kutabasamu kimoyo moyo na kujiona wewe ni bonge la mjanja ila wakati wako tu ndio haujafika.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]eti kindi-tandahimba

Back
Top Bottom