Redioni na kwenye magazeti kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu huu ugonjwa. Kirefu sahihi cha UTI ni URINARY TRACT INFECTION. Siyo TRACK. Wapotoshaji wakubwa ni hawa wanaojiita madaktari wa matibabu mbadala, matapeli wakubwa sana. Wengine wanaenda mbali na kusema ati UTI inaweza kutibiwa kwa kupata dawa mara moja tu. UTI ni ugonjwa wa wote, wanaume na wanawake. Ila wanawake wanaugua mara nyingi zaidi kuliko wanaume.
Ukweli ni kwamba hakuna daktari wa matibabu mbadala anayeweza kutibu UTI.
Tatizo lipo kwa serkali kupitia kwa wizara ya afya kuwaruhusu hawa wapotoshaji/matapeli kujitangaza. Radio wanazozitumia zinajali pesa tu.
UTI isipotibiwa haraka ina madhara makubwa sana, hasa kwa wanawake.
Kwa sababu ya kuongezeka kwa matapeli wa matibabu hivi karibuni, sasa hivi UTI umekuwa ugonjwa common sana kuliko uhalisia.
Kama uko Dar na unahisi una UTI, nenda MUHAS kaonane na Dr wa idara ya Microbiology, au nenda idara ya Internal Medicine. Tatizo ukiwa mikoani.
Hawa matapeli wanatumia vibaya uelewa mdogo (ignorance) ya wa TZ walio wengi.