Mnaosema eti huna haja ya kumchunguza mwenzio fikirieni tena. Ukiwa huna haja ya kumchunguza ujue hakuna tatizo. Ila kama kuna tatizo, ujue mambo huwa hayawi kawaida ndo maana unalazimika kuanza kuchunguza. Kwa kifupi akiwa anatoka (Mke au mme) lazima wewe ambaye hutoki utaathirika na tabia yake hiyo. Mfano mwanamke akitoka kwa mwanaume mwingine hata usipochunguza, atakufanyia vitu ambavyo huvitarajii. Huduma inaweza kukauka kabisa, hata akifanya analipua tu ili umalize uondoke. Heshima hupungua au huisha kabisa na magomvi yasiyo na sababu huzuka muda wowote bila hata kutarajia.
Kwa mfano ukiwa na usafiri, yuko sehemu anakwambia njoo unichukue. Unakwenda, anakuweka saa nzima, halafu akitoke ukamuuliza imekuwaje akugandishe saa nzima, hana maelezo ila anafoka tu au anazira kabisa hataki tena kupanda lift yako! Anaweza kuchelewa kurudi bila sababu, ukiuliza unaambulia matusi au kununiwa wiki nzima.
Baada ya hayo yote, napenda nikubaliane na mtambuzi kwa asilimia mia moja!! Hili ni jambo ambalo nimeliona na nilithibitisha! Dalili zoote alizotaja mtambuzi niliziona. Kifupi, sasa hivi tuna wind-up ndoa ya miaka 13!