Jamani hapa huwa watu siwaelewi..utaona leo amekuja na ..Dalili za wana-me/ke wanaotoka nje ya ndoa, mala dalili za demu changudoa, nahitaji jimama la kunipa raha...
Jamani haya yote ya nini? kwa nini tusiishi kama moyo wako unavyokutuma? ishi wewe kama wewe usimtegemee mtu yeyote aje hapa akushauri kitu na wewe bila kuchunguza ukweli wake unakurupuka na ku-ACt on it! haya hizo dalili ulizozitoa hapo juu utaona watu wanaanza kuwachunguza wake zao....leo mke amesahau pete yake tayari mume anaanza kuuliza, leo kachelewa saluni bila hata kufikiria labda alipitia kwenye mambo yake mengine kama wewe unavyopitaga tayari njembe inaanza kuquestion, leo kakutana na rafiki yake wa kike wakaenda soko lingine wakachelewa tayari unachunguza....ukichunguza chunguza utapata pressure bure na ufe mapema.
My Take: uwe umeoa/umeolewa ishi wewe kama wewe na uishi na mwenza wako kwa akili kama biblia ilivyosema " na nyinyi waume muishi na wake zenu kwa akiri" na hiyo si kuishi kwa kumchunguza pls pls?