DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mbunge mteule wa Viti Maalumu kupitia kundi la Vijana, Ng’asi Damas Kamani, amempongeza Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa hatua kubwa alizochukua katika kutatua changamoto za vijana nchini, hususan katika sekta za ajira, elimu, na uwezeshaji kiuchumi.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Mwanza, leo Jumatano Oktoba 8, 2025, Kamani amesema Dkt. Samia ametekeleza ahadi alizotoa kwa vijana kwa kiwango kinachozidi asilimia mia moja.
“Katika uwanja huu huu uliwahi kuja kuzungumza nasi vijana wa Tanzania, na yote uliyoahidi umetekeleza kwa zaidi ya asilimia mia moja. Ulituahidi ajira milioni nane, na ninayo furaha kusema umetimiza zaidi ya ahadi hiyo — ajira milioni nane, elfu themanini na nne, mia mbili na tatu katika kipindi cha miaka minne. Nani kama Dkt. Samia?” amesema Kamani huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Ameongeza kuwa vijana wa Mwanza wamenufaika kwa kiasi kikubwa kupitia miradi ya kiuchumi inayohusisha ufugaji wa samaki katika vizimba na uvuvi wa kisasa.
“Hapa Mwanza tuna Ziwa Viktoria, na zaidi ya vizimba 508 pamoja na boti zaidi ya 200 vilivyokabidhiwa na Rais Samia. Vijana wengi wamepiga hatua kubwa kimaisha kupitia miradi hii,” amefafanua.