Damas Ndumbaro atupwa jela ya soka miaka 7

Damas Ndumbaro atupwa jela ya soka miaka 7

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.

Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa hadharani na vilabu huku vikisema kuwa havikumtuma kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa utashi wake mwenyewe, na si wao walimtuma.

Kilichomuhuku ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe.

ShaffihDauda

NDUMBAROO.jpg
NDUMBBA.jpg
NDUBALO2.jpg
NDUMBA.jpg
 
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.

Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na
havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye
alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa hadharani na vilabu huku vikisema kuwa havikumtuma
kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa utashi wake mwenyewe, na si
wao walimtuma. Kilichomuhuku ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu.

Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe. 

source: shaffih Dauda
 
Aliongea kwa 'utashi' wake!!! ina maana hakutumwa na vilabu kuongea yale aliyoyaongea? Mmmmmmmmh! mbona hii haiji kiakil au kuna mchezo umechezwa hapa! Soka la bongo lina mizengwe, Ngoja tutamsikia Ndumbalo atasemaje.
 
Wabura huko aliko atakuwa ameupokea uamuzi huu kwa nderemo na vifijo waandishi jaribuni kumtafuta wabura anasemaje juu ya maamuzi haya ya kamati ya nidhamu zidi ya bwana Ndumbaro
 
Wabura huko aliko atakuwa ameupokea uamuzi huu kwa nderemo na vifijo waandishi jaribuni kumtafuta wabura anasemaje juu ya maamuzi haya ya kamati ya nidhamu zidi ya bwana Ndumbaro

Mbaya wake "kang'olewa meno" ama kweli uishi kwa makini kwani hujui kesho yako ikoje au vipi mkuu NAPITA
 
Last edited by a moderator:
Fanya hivyo hivyo mpinzani na ikiwezekana hata zile sare wasipate wafungwe tu.
mkuu mkolaj yaani Wazee wa kamati ya fitna na ufitinishi huwa hawaishiwi "comprehensive startegic planning" kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Hivi wakili hawezi kufungiwa yeye anatetea vilabu, wangevifungia vilabu kwanini TFF inalazimisha kuchukua fedha za vilabu.
 
Hivi wakili hawezi kufungiwa yeye anatetea vilabu, wangevifungia vilabu kwanini TFF inalazimisha kuchukua fedha za vilabu

Mbona vilabu kama vimemkana kiaina flani vile au habari inasomekaje mkuu tracy martins
 
Last edited by a moderator:
Sina wacwc ninachoamini wakili ana akili kuna njia ambazo atapita hayo maamuzi yatatenguliwa hizo hukumu za kimtaani na influence mara nyingi hazina mantiki ktk sheria!!!!!!
 
Back
Top Bottom