Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mh Damas Ndumbaro ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria , ametamka hadharani kwamba zaidi ya 50% hawaijui Katiba ya sasa , Kwa tafsiri ya Kawaida ni kwamba zaidi ya nusu ya Wananchi hawaijui Katiba yao .
Kumuamini Ndumbaro kunahitaji roho ngumu iliyojaa Ujasiri wa kutukuka , Ndumbaro amewahi kuwa Wakala wa wachezaji wa FIFA , ambaye alifungiwa kushiriki masuala ya soka na Wachezaji kwa muda usiojulikana kwa UDANGANYIFU NA UTAPELI, tunawezaje kumuamini mtu huyu ?
Tanzania kuna watu wazima , Vijana na watoto , hawa ndio wanaounda 100% ya raia wote , na humo wamo ambao kwa umri wao na utoto wao kwa namna yoyote ile hawawezi kujua lolote lile kuhusu Katiba ya nchi , hawa nao wamo kwenye hiyo 50% ya wasioifahamu Katiba ya sasa?
Hata kama Waziri anatunga Uongo ili kuikwepa Katiba Mpya kwa lengo la kuokoa ccm , basi Ajitahidi kuupaka rangi uongo wake , kama kweli watanzani wote hao hawajui Katiba yao basi athibitishe namna alivyokokotoa hesabu hiyo ndani ya siku mbili au tatu za kuandaa huo uongo wake , alimhoji nani na yupi , wapi na lini ? aweke ushahidi mezani tuuone.
Hivi waliompa Uwaziri wa Sheria Ndumbaro walizingatia vitu gani ? mbona ni mwepesi sana ! ccm haina watu wengine wenye weledi hadi kutafuta mtu mwenye makandokando kama huyu , asiyejua juzi na jana aliongea nini ? huyu huyu aliwahi kudanganya kwamba Mchakato wa Katiba mpya utaanza Septemba (Ushahidi uko humu jf) , wakati akiyasema haya hawa Watanzania Mbumbumbu wa Katiba walikuwa % ngapi ?
Naomba nifupishe kwa kusema hivi KATIBA MPYA NI SASA na wala si baada ya miaka mitatu anayoitaka Ndumbaro na waliomtuma , PATACHIMBIKA .