MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Shirika la Habari la Serikali ya Syria,SANAA limeripoti kwamba,Msafara wa wanajeshi kadhaa wa Urusi pamoja na vifaa vya kijeshi vimeanza kuondoka nchini Syria.
Video kadhaa zimeonesha msafara wa magari ya kijeshi ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga aina ya S-300/400, Vifaru aina ya T-64 na Magari ya kubeba Silaha yakiondoka kutoka eneo la KHMEIMIM AIRBASE iliyoko katika ufukwe wa Bahari ya Mediterannea.
Kumekuwa na mazungumzo kadhaa ya siri kati ya Uturuki na Urusi wa kuiruhusu Urusi kupitisha misafara ya wanajeshi wake na vifaa vya kijeshi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Uturuki nchini Syria ili kuwarudisha nchini Urusi. Hii ni baada ya Waasi wa kundi la HTS kuipindua serikali ya Bashar Al Assad Mshirika wa Iran na Urus na kumlazimu kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Urusi mnamo Desemba 08.
Urusi ilikuwa na wanajeshi wanaokadiriwa 12,000 nchini Syria tangu mwaka 2015 ilipojiingiza kijeshi nchini Syria ili kumsaidia Assad kupambana na waasi waliotaka kuiteka nchi hiyo. Hata hivyo,Baada ya Urusi kuivamia nchi ya Ukraine,Urusi iliwapunguza wanajeshi wake kutoka Syria kuwapeleka uwanja wa vita nchini Ukraine. Mpaka sasa,Urusi ilikuwa na wanajeshi wafikao 5,000 nchini Syria wengi wao wakiwa ni Washauri wa Kijeshi waliokuwa wakitoa mafunzo kwa jeshi la Syria tangu mwaka 2015.
View: https://youtube.com/shorts/nzwQYRddFAY?si=wn1CEHPgA5PK36Ex