Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Mwisho wa vita moja ni mwanzo wa vita nyingine

Nimefurahi kuona Iran amerudishwa Nyuma, Now IRGC watabidi wafanye kazi zao wakiwa Iraq na Lebanon hawatapata tena Silaha hadi ushirikiano wao Na Kobazi wengine uimarike.

What next, Uturuki anaenda kuwa Kiranja wa Waarabu na Wanamgambo wake wapya wanaenda kuwa mpakani mwa Israel, hii ni changamoto mpya,

Effect ya kuanguka kwa Assad kutachochea vuguvugu la Wassuni na Muslim brotherhood kwenye Mataifa mengine ya kiarabu linaweza kukua sana.

Russia asikubali kupoteza kambi zake za Kijeshi Syria, in short asifanye mambo kama punga, badala yake aforce Syria igawanywe kimafungu, ataungwa Mkono na Israel, Iran(atakubali fedaration ambayo Wakurd watakuwa huru bila nchi), USA, Wakurd, Waarabu wa Kidruze, Kikristo na mataifa mengi ya Ulaya na Yenye nguvu, Chawa wa Russia nao wakubali hii proposal, Atapingwa na Mataifa yote ya Kissuni, yakiongozwa na Uturuki
 
aljazeeraenglish-20241208-0001.jpg
 
BREAKING NEWS

Waasi wa HTS tayari wameuteka mji wa HOMS ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Syria. Wakati hayo yakiendelea,Kundi moja la waasi wa HTS limeuzingira mji wa Damascus kutokea kusini huku kundi lingine lililouteka mji wa HOMS likitokea Kasikazini kuelekea Damascus na hivyo mji huo kuzingirwa pande zote mbili za Kusini na Kasikazini.

Rais Bashar Al Assad ameahirisha kulihutubia taifa kama ilivyokuwa imepangwa. Ripoti zinasema,rais huyo ameikimbia nchi hiyo na kwenda Kutengeneza Serikali yake ya Mpito huko Ng'ambo,ambapo atalihutubia taifa akiwa huko. Taarifa zinadai huenda rais huyo amepewa hifadhi ya kisiasa nchini Urusi au Iran.

Jeshi la Israel kwa upande wake limetuma vikosi vyake vya ardhini nchini Syria kutokea Milima ya Golan na kuteka vijiji kadhaa vilivyokuwa chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa.

 
BREAKING NEWS

Waasi wa HTS wametangaza kuuteka mji mkuu wa Syria Damascus. Pia wametangaza kukimbia kwa rais wa nchi hiyo kwenda uhamishoni.

Kiongozi wa waasi amewataka wote walioikimbia nchi ya Syria kwasababu ya utawala dharimu wa Assad na vibaraka wake wa Urusi na Iran waanze kurudi Nyumbani.
 
UPDATES FROM SYRIA

Kiongozi wa Waasi wa HTS ametangaza kwamba,Idara zote za Serikali isipokuwa Wizara ya ulinzi zitakuwa chini ya Waziri mkuu wa Syria mpaka hapo itakapotangazwa rasmi serikali mpya ya nchi hiyo.

Hii ni baada ya Serikali ya awali ya Bashar Al Assad kuangushwa na waasi wa HTS, na hivyo kumfanya Rais Assad kuikimbia nchi hiyo?
 
Kwa hio kila anaye wapa support Israel na US huyo ndio mnampenda sio. Unataka kusema huyo mpiganaji wa Al Qaeda kapata vipi connection na US na Israel. Afu US anakuambia hao magaidi na wakati anawapa support. Tukiwambia dunia bila US na Israel kungekiwa na amani mnabisha
kwan nyiny waislam hamuna akil mpk muendeshwe na USA na ISRAEL?
 
Kasema ameachana na Ugaidi na ametubu kwa Allah na Serikali yake itakuwa ni Inclusive Madhehebu yote ya Kiislamu Madhehebu yote ya Kikristo na Wayahudi wa Syria pia watahusishwa kwenye Serikali yake mpya.
Hii ndo tunayo itaka
Uhuru wa kuabudu
Kituo kinachofuata ni Iran tumalizia kwa kiduku 😄😄😄
 
Back
Top Bottom