JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Hapana shaka afya za wakazi wa Dar es Salaam na Pwani, zipo hatarini. Hii ni kutokana na kuuziwa matunda yanayookotwa katika Dampo hili ambalo wenyeji wa maeneo husika ya Kata ya Vikindu, Mkuranga mkoa wa Pwani, wanaamini mmiliki wa Dampo ni Bakhresa Group. Matunda yanayotupwa hapa, huokotwa na kuuzwa katika masoko mbalimbali likiwemo soko la Stereo, Temeke.
Kadri unavyokaribia eneo lililopo Dampo hili, unakumbana na harufu kali ambayo ni vigumu kuivumilia, hasa unapokuwa mgeni. Mmoja wa Wakazi wa eneo hilo anasema “Pamoja na hali hiyo, sisi wenyeji kuna muda hatuisikii harufu. Wageni wakifika, ndiyo huwa wanatushitua kuwa hali si nzuri. Hiyo ni dalili kuwa tumeathirika, lakini hatujui…”
Picha mbalimbali zikionesha mazingira ya Dampo la Bakhresa ambapo asilimia kubwa ya taka zinazoonekana ni matunda kutoka kwenye kiwanda cha juisi mali ya mmiliki.
Hata hivyo, wakati wa mvua nyingi au taka zinapoletwa kwenye dampo hilo hata Wenyeji ambao huwa hatusikii harufu kutokana na kuzoea mazingira, husikia harufu kwa ukali zaidi hatua inayowafanya watambue kuwa hali ya mambo si nzuri kabisa.
Dampo halina wadudu, nini kinawekwa?
Jambo la kushangaza katika Dampo hilo ni kutokuwepo kwa Wadudu. Ni kawaida ya sehemu za taka kukuta wadudu kama Nzi na Funza lakini kwa Dampo la ‘Bakhresa’ hali ni tofauti. Licha ya taka nyingi hasa za maembe zinazotupwa eneo hilo na kutoa harufu kali ya kuoza hakuna mdudu hata Nzi wanaokaa kwenye dampo hilo. Wananchi wa eneo hilo wanajiuliza; Je, wanaotupa taka wanaweka dawa au kemikali gani hizo?
Malalamiko ya wakazi na kinachotokea
Baadhi ya Wakazi wa eneo hilo wanasema “Sisi Wananchi kwa kushirikiana na uongozi wa Serikali za Mitaa, tumeshaenda mara kadhaa kwa wamiliki wa Dampo kuwaambia waweke uzio, angalau kuzuia watu kuingia hovyo kwenye Dampo. Hilo halijafanyika wanapuuzia.”
Anaongeza “Kuna watoto wanaoenda kucheza ndani ya Dampo, kitu ambacho ni hatari kiafya. Kibaya zaidi, baadhi yao wanaokota maembe yanayotupwa hapo, hasa yale yanayoonekana kuwa na hali nzuri, wanayala. Wengine wanaokota na kwenda kufanya biashara ya kuyauza mtaani.”
Wakazi hao wanasema Wanaookota matunda hayo hawawauzii watu wa mtaani hapo, kwa kuwa wanajua wanachokifanya. Wengi wanaenda kuuza Mbagala na Temeke. Mengi ni yale maembe ambayo yanauzwa kimafungu, kwa bei rahisi, na mengine yanatengenezewa juisi zinazouzwa mitaani
Lakini pia Wakazi hao wanalalamika kuwa sehemu ya dampo hilo imeinama hivyo wakati wa mvua, uchafu unaotoka Dampo unaelekea kwenye mfereji wa maji ambayo yanaelekea kwenye makazi yetu.
Kuna wakati baadhi ya Wananchi wanayachota hayo maji kwa matumizi mbalimbali. Maji mengine yanaelekea kwenye mto, kisha baharini. Wananchi wanajiuliza, hizo kemikali ambazo hata Nzi, Funza au Sisimizi hagusi, zinaenda kwenye maji yanayotumiwa na watu, madhara yake ni nini?
Watoto katika Dampo hilo.
Si Watoto na Wakazi pekee wanaookota Maembe na kwenda kuuza
Magari ya Bakhresa yanapomaliza kutupa taka (matunda yaliyokataliwa kiwandani), kuna baadhi ya watu huwa wanakuja na magari na kuanza kuchagua matunda wanayoona yanafaa, wanayaweka kwenye magari yao na kuondoka nayo.
Wanakijiji wanasema “Tunawajua sura na magari yao wanayotatumia kuja kukusanya maembe, lakini hatuwezi kuwataja kwa usalama wa maisha yetu, kwa kuwa hayo ndio maisha yao. Ndio maana, Kipindupindu na magonjwa mengine hasa ya tumbo huwa hayaishi Dar es Salaam na Pwani.”