Dampo hilo hivi karibuni liliripotiwa kukithiri kwa uchafu ambapo wahusika hawakuwa wakichukua hatua ya kuzuia tahadhari ya usalama wa afya wa Watu waliopo eneo hilo, lakini nimepita hapo nimeshuhudia mazingira yamekuwa sai tofauti na ilivyokuwa awali.
Soko hili ambalo lilo katikati ya mji linaangaliwa kwa ukaribu, hivyo kuepusha uchafu kujaa hadi barabarani ni uamuzi wa busara.
Uchafu uliokuwepo ulikuwa ni moja ya hatari ya kuwa na maambukizi ya milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.
Wakiendelea hivyo naamini kila kitu kitakuwa safi, niwapongeze waliowajibika lakini nipongeze pia JamiiForums kwa kupaza sauti juu ya eneo hilo.
Hali ilivyokuwa awali ~ Manispaa ya Singida iangalie Dampo la Msufini, linatunzwa vibaya na ni hatari kwa Afya