Dampo la Msufini hatimaye limesafishwa, mazingira sasa yamekuwa masafi

 Dampo la Msufini hatimaye limesafishwa, mazingira sasa yamekuwa masafi

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Soko la Msufini lililopo eneo la Msufini katika Manispaa ya Singida hivi karibuni kulikuwa na changamoto ya uchafu katika sehemu ambayo ilifikia hatua ya kuitwa Dampo la Msufini.

Dampo hilo hivi karibuni liliripotiwa kukithiri kwa uchafu ambapo wahusika hawakuwa wakichukua hatua ya kuzuia tahadhari ya usalama wa afya wa Watu waliopo eneo hilo, lakini nimepita hapo nimeshuhudia mazingira yamekuwa sai tofauti na ilivyokuwa awali.

Soko hili ambalo lilo katikati ya mji linaangaliwa kwa ukaribu, hivyo kuepusha uchafu kujaa hadi barabarani ni uamuzi wa busara.

Uchafu uliokuwepo ulikuwa ni moja ya hatari ya kuwa na maambukizi ya milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.

Wakiendelea hivyo naamini kila kitu kitakuwa safi, niwapongeze waliowajibika lakini nipongeze pia JamiiForums kwa kupaza sauti juu ya eneo hilo.
20241126_133600.jpg

20241126_135656.jpg

Hali ilivyokuwa awali ~ Manispaa ya Singida iangalie Dampo la Msufini, linatunzwa vibaya na ni hatari kwa Afya
 
Back
Top Bottom