A
Anonymous
Guest
Kero yetu ni uwepo wa dampo kubwa la takataka katika Kata ya Murubona, Wilaya Kasulu Mji, dampo hilo ni hatarishi kwa jamii inayozukwa na taka kwani ni chanzo kikubwa cha magojwa, lilianzishwa hapo Mwaka 2023.
Harufu mbaya ya taka, wadudu wasumbufu imekuwa tatizo kubwa.jambo hili linakingiwa kifua na viongozi wapenda rusha ambao hawapeleki malalamiko ya wanamtaa kwa mamlaka husika, watu wao ni Mwenyekiti wa Mtaa.
Bwana afya wa Mji Kasulu pia Mkurugenzi wa Mji Kasulu kwa kushindwa kufuatilia mahitaji ya raia wake wote hao wamekuwa upande mmoja wa mkusanya taka badala ya kutetea maslahi ya jamii inayoteseka.
Awali eneo hilo lilikuwa ni open space, maeneo ya wazi kwa ajili ya maeneo ya akiba, hali hiyo ya kuwekwa kwa taka ilianza baada ya mamlaka ya mji kumruhusu mkusanyaji taka kupewa idhini ya kumwaga eneo hilo.