Dampo lililopo Kilimahewa hapa Morogoro linatutesa Wananchi

Dampo lililopo Kilimahewa hapa Morogoro linatutesa Wananchi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
WhatsApp Image 2024-10-04 at 08.52.21_ccd731b8.jpg
Mimi ni mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa, Kata ya Mafisa Manispaaa ya Morogoro huku kwetu kuna Dampo ambalo halitunzwi vizuri na uchafu wake umekuwa ukisambaa maeneo tofauti hali ambayo inaweza kusababisha kutokea kwa magojwa ya Mlipuko.

Hili Dampo limekuwa ni kero sana, taka zinazagaa barabarani na nyingine kwenye makazi ya Watu hali hii ni mbaya sana tunahofia kupata magojwa ya mlipuko.
WhatsApp Image 2024-10-04 at 08.52.21_47abdafb.jpg

WhatsApp Image 2024-10-04 at 08.52.21_157db5bc.jpg
Nzi ni wengi na wanatusumbua, harufu ni mbaya mpaka tunashindwa kula chakula, tunaiomba Mamlaka husika hasa Manispaa kupitia kitengo cha mazingira watusaidie kulihamisha Dampo hili kwani lilitengwa tangu Mwaka 1998, sasa hivi lishazungukwa na makazi ya Watu ni hatari.

Ubaya zaidi tushaiwasilisha hii changamoto kwa Manispaa lakini bado halifanyiwi kazi, tunaomba JamiiForums mtusaidie kupaza hii sauti, tuna.

Hapa mvua zikianza kukchanganya hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa kuwa uchafu umesambaa hadi barabarani.

Pia, Soma
==> Dampo katika Soko la Stereo lililopo Temeke ni kero kubwa, Mamlaka ziongeze nguvu katika kuzoa taka
==> Dampo la ‘Bakhresa’ Mkuranga, linahatarisha afya za wakazi Dar na Pwani. Matunda kutoka dampo hilo yauzwa tena sokoni
==> RC Malima: Kama Morogoro mnataka kuwa Jiji acheni uchafu na ongezeni makusanyo ya Nndani
 
Back
Top Bottom