Eneo hilo linalotupwa taka ni bonde, hivyo wakazi wa hapo waliiomba Manispaa ya Kinondoni wawe wanatupa taka hapo kwa nia ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi kwakuwa eneo hilo ni bonde.
Makubaliano yalikuwa taka zitupwe bondeni lakini pia zitupwe kwa usafi kwa kupigwa dawa na kuzisawazisha ili zisilete madhara ya kiafya kwa Wakazi wa eneo hilo.
Manispaa imeshindwa kuzingatia hilo jambo muhimu kama hilo matokeo yake watupa taka wakifika hapo wanatupa njiani yaani pembeni ya bonde ambapo taka zinazagaa ad barabarani.
Wenyeji wanasema wakifika hapo wanazimwaga na kuondoka bila kuzingatia wala kujali afya ya binadamu.
Madhara ya jambo hili ni mchafuko wa hali ya hewa, eneo hili lina harufu nzito na kali ambayo inaweza kusababisha athari ya afya kwa binadamu hasa watoto.
Ikifika majira ya Saa Sita au Saba jua likiwa kali sana harufu inaenea maeneo yote ya mitaa hiyo jambo linaloleta kero kwa Watu.
Harufu ni kali na hewa ni nzito, hivyo wakati mwingine Watu wanakosa hewa safi.
Jambo hili linapaswa kuchukuliwa hatua na mamlka husika kwa haraka ikiwa wanashindwa kutunza mazingira ya dampo hilo basi walipige dawa na kulifunga ili kuepusha madhara makubwa baadaye.