Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mkeo na watoto wako ni ndugu zakoHabarini wana JF!
Katika makuzi kila mmoja wetu amekua akiambiwa waheshimu ndugu zako wa damu, maana damu ni nzito kuliko maji! na hakika huu msemo unamake some sense, mpk mtu utakapo kuwa na kuanza kujitambua.
Ukweli usemwe kuna misemo mingine mababu zetu walikunywa gongo mbaya kabisa kupindi wanaiunda. Hasa huu wa damu ni nzito kuliko maji, umewafanya watu wengi sana kuteseka, kudharaulika, kutengwa na wengine hata kujiua.
Neno ndugu linamkanganyiko mkubwa sana hasa kama ukiliamini asilimia šÆ. Ndugu wa kweli sio yule wa damu bali ni yule ambaye ajengae mahusiano yenye afya nawe. Kama mtu umuitaye ndugu wa damu na ndo chanzo cha wewe kukosa furaha basi huyo si ndugu! Neno ndugu lapaswa liangaliwe vizuri watu wengi wameingia kwenye matatizo.
Labda zamani, maana kidogo watu walikua na maadili ila sasa ndugu si mpaka awe wa damu. Hakuna maana tena yenye kuthaminisha hilo neno. Hasa tukiangalia watu walivyo telekezwa na kuachwa na hao watu waitwao ndugu wa damu. Kamwe sitakubalina na hii dhana ya damu ni nzito kuliko maji. Hao ndugu ndo watu wa kwanza kukutakia mabaya na kukufanyia fitna usifanikiwe.
Simaanishi ndugu wote ni wabaya, ila huo msemo hauna mantiki kwa generation tuishio sasa.
Nakubaliana nawe hii mentality hata mm ninayo ya kuto ku connotate maana ya neno husika based on societal norms. Umesema kuwa ndugu ni bloodline na sio malaika which is so correct.Mkuu mkeo na watoto wako ni ndugu zako
Mama, baba, kaka na dada zako ni ndugu zako...... Hawa watu wanaweza kuwa wema kwako au washenzi kwako kama wanavyoweza kuwa watu wengine wowote
Ila utaumia sana ukifanyiwa ushenzi na mtu baki kuliko ndugu yako
Sasa hapo inategemea na uwezo wako wa kuchakata na kutafsiri methali
Kama unatafsiri ndugu ni lazima wawe malaika kwako basi utakua sahihi
Lakini utatafsiri ndugu ni binadamu kama binadamu wengine utabaini methali inamshiko
Kuna sababu kwanini hakimu jaji haruhusiwi kushughulika na kesi inayomuhusu ndugu
Kuna sababu kwanini ufalme ulikua unarithishwa kindugu
Kuna sababu kwanini mali za marehemu zinarithiwa na ndugu
Kuna sababu kwanini tunatumia majina ya ukoo nk nk
Mkuu sijui unapitia mapito gani na ndugu zako lakini ukweli ni kwamba pale dunia nzima itakaposhindwa kusimama na wewe ni ndugu zako pekee watakao simama na wewe hadi mwisho wako..... haijalishi mnapitia hali ganiNakubaliana nawe hii mentality hata mm ninayo ya kuto ku connotate maana ya neno husika based on societal norms. Umesema kuwa ndugu ni bloodline na sio malaika which is so correct.
Ndo maana nilisema neno ndugu lapaswa kuamngaliwa kwa makini maana kuna kama vile connection ambayo watu tumejiwekea kuhusu ndugu, hii imesababishia wengi changamoto na kushindwa kuishi maisha yaliyo na furaha simply bcoz wanataka kufurahisha ndugu.
Kuna umuhimu wa kuwa na ndugu kama ulivyo taja hapo pia ina leta identity na sense of originality. Lakini jinsi tunavyotakiwa kurelate na ndugu ndo kunamtihani kwa wengi. Japo ndugu apaswa kua kipaumbele ila sio in all circumstances.
Utasikia subira yavuta kheri wakivurugwa utasikia ngoja ngoja yaumiza matumboššHawa wazee jau sana, wanakwambia HARAKA HARAKA HAINA BARAKA ukiwa na jambo lako, wakiwa na jambo lao wanatumia NGOJA NGOJA YAUMIZA MATUMBO.