Damu sio nzito kuliko maji

Hawa wazee jau sana, wanakwambia HARAKA HARAKA HAINA BARAKA ukiwa na jambo lako, wakiwa na jambo lao wanatumia NGOJA NGOJA YAUMIZA MATUMBO.
Wanatuchanganya sana🤣... mpk uwe na hekima kuchuja.
 
Mkuu mkeo na watoto wako ni ndugu zako
Mama, baba, kaka na dada zako ni ndugu zako...... Hawa watu wanaweza kuwa wema kwako au washenzi kwako kama wanavyoweza kuwa watu wengine wowote
Ila utaumia sana ukifanyiwa ushenzi na mtu baki kuliko ndugu yako

Sasa hapo inategemea na uwezo wako wa kuchakata na kutafsiri methali
Kama unatafsiri ndugu ni lazima wawe malaika kwako basi utakua sahihi
Lakini utatafsiri ndugu ni binadamu kama binadamu wengine utabaini methali inamshiko

Kuna sababu kwanini hakimu jaji haruhusiwi kushughulika na kesi inayomuhusu ndugu
Kuna sababu kwanini ufalme ulikua unarithishwa kindugu
Kuna sababu kwanini mali za marehemu zinarithiwa na ndugu
Kuna sababu kwanini tunatumia majina ya ukoo nk nk
 
Nakubaliana nawe hii mentality hata mm ninayo ya kuto ku connotate maana ya neno husika based on societal norms. Umesema kuwa ndugu ni bloodline na sio malaika which is so correct.

Ndo maana nilisema neno ndugu lapaswa kuamngaliwa kwa makini maana kuna kama vile connection ambayo watu tumejiwekea kuhusu ndugu, hii imesababishia wengi changamoto na kushindwa kuishi maisha yaliyo na furaha simply bcoz wanataka kufurahisha ndugu.

Kuna umuhimu wa kuwa na ndugu kama ulivyo taja hapo pia ina leta identity na sense of originality. Lakini jinsi tunavyotakiwa kurelate na ndugu ndo kunamtihani kwa wengi. Japo ndugu apaswa kua kipaumbele ila sio in all circumstances.
 
Mkuu sijui unapitia mapito gani na ndugu zako lakini ukweli ni kwamba pale dunia nzima itakaposhindwa kusimama na wewe ni ndugu zako pekee watakao simama na wewe hadi mwisho wako..... haijalishi mnapitia hali gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…