SI KWELI Damu yenye Maambukizi ya Magonjwa hutunzwa baada ya kukusanywa kutoka kwa wachangiaji ili wawekewe watu wenye Magonjwa husika

SI KWELI Damu yenye Maambukizi ya Magonjwa hutunzwa baada ya kukusanywa kutoka kwa wachangiaji ili wawekewe watu wenye Magonjwa husika

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Habari,

Ninanukuu kutoka kwenye meseji iiyotummwa kwenye kundi moja la Telegram ambalo mimi pia nimo.

Huku mitaani kuna taarifa kuwa kuwa uvunaji wa damu unaifanyika maeneo mbalimbali nchi huwa siku hizi hawatupi damu yoyote hata kama wataikuta ina ugonjwa wowote kwa kuwa damu hiyo wata muongezea mtu mwenye ugonjwa ulipo kwenye damu, mfano wakakuta damu waliyovuna ina virusi vya ukimwi hawaitupi akija mgonjwa mwenye ukimwi basi wata muongezea damu hiyo je hii ni kweli?

Inasadikika hili limechangiwa na ugumu wa kupata damu lakini pia hakuna shida yoyote mfano mtu ana virusi vya UKIMWI akiongezewa damu ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa tatizo lake hapo ni damu si salama au isiyo salama, eti hata kama wangemuongezea damu iliyo salama bado damu hiyo ikisha ingia mwilini mwake haita kuwa salama kwa kuwa muhusika tayari ana virusi vya ukimwi, je hii ni kweli?

Mtusaidie maana mimi naogopa sana, na hii inasadikika ni kwa magonjwa yote kuwa damu iliyo vunwa na si salama haitupwi bali ataongezewa mtu mwenye ugonjwa huohuo.

shutterstock-medium-file[1].jpg
 
Tunachokijua
Hadi sasa hakuna utaalamu wa kuzalisha damu nje ya binadamu hivyo watu wanapojitolea damu hushiriki kikamilifu katika mnyororo wa kuokoa maisha ya watu wengine.

Baada ya kukusanywa kwake, damu hii hupimwa Kiwango cha damu, UKIMWI (VVU), Kaswende, Homa ya Ini (Hepatitis B na C) na Makundi ya damu. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Mchakato huu wa ukusanyaji na upimaji wa damu umezua maswali ambapo kwa mujibu wa muanzisha mada, baada ya damu hii kugundulika na magonjwa tajwa huhifadhiwa ili watu wenye magonjwa husika waweze kupatiwa.

Aidha, kwa mujibu wake, kitu hiki kinachagiwa na uhaba wa damu uliopo Tanzania na duniani kote hivyo ili kukidhi haya ya mahitaji, damu hii hutumika tena kwa watu.

Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imezungumza na Mr. Dunstan Haule, Mkuu wa Idara ya Viwango na Ubora Mpango wa Taifa wa Damu Salama wenye jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote za usalama wa damu nchini ambazo ni pamoja na upatikanaji wa wachangiaji damu wa hiari, ukusanyaji wa damu kutoka kwa wachangiaji wa damu wanaostahili, uhifadhi wa damu, utengenezaji wa mazao ya damu, upimaji wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya damu (TTIs), upimaji kwa serolojia ya makundi ya damu na ugavi wa damu salama na mazao ya damu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya aliyekanusha madai haya na kuyaita ni Uzushi.

"Ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho, mgonjwa yeyote anapata damu salama kwa maana ya damu salama. Damu yeyote ambayo imegundulika kuwa na maambukizi au kutokidhi ubora inateketezwa mara moja." amesema Haule.

Aidha, miongozo ya taasisi zingine duniani inakazia pia suala hili la kuteketeza damu zenye maambukizi baada ya kuvunwa kutoka kwa wachangiaji. Mathalani, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeweka mwongozo huo unaotaka kuharibiwa kwa damu baada ya kukutwa na maambukizi ya magonjwa.

"Ikiwa kwenye mchakato wa ukusanyaji damu yoyote itaonekana kuwa na maambukizi ya Magonjwa, mhusika hujulishwa lakini damu husika huondolewa kwenye utaratibu wa kupewa mtu mwingine", imeandika pia Taasisi ya NHS.
Back
Top Bottom