Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hiyo Tanzania kuwa na mapori ni mengi ni uongo mkubwa na propaganda tu. Na wenye akili wengi pia wanazungumza wageni kuchukua maeneo yenye madini, gesi na mafuta. Tanzania wako watu milioni 60 na wanazidi kuongezeka kwa kasi, hayo mapori mengi yanatoka wapi??
Tanzania mapori mengi sana, hata wewe ukiwa na hela unanunua ekari utakazo.
Kama kuna maeneo ekari moja inauzwa mpaka laki moja na zipo nyingi hazina hata wanunuzi shida iko wapi, hapo tu mbwewe, msata, hiyo kiwangwa, hapo kidomole nk ambapo ni karibu na Dar ardhi ekari moja inauzwa laki tano na maeneo mpaka kesho yapo yakumwaga.
WaAfrica wengi wetu akili zetu fupi sana, leo hii ukiwaambia watu wakalima kwenye mashamba yao ya urithi wanaleta blah blah na yamebaki mapoli tu huko, akija Mzungu au Mgeni akanunua ardhi hiyo hiyo, ng'a ng'a za kumwaga.
Matajiri wetu wenyewe wenye hela wanachoweza ni kujenga bar, night clubs, mahoteli, guest house katikati ya mji na kuwa wanasiasa, wakija wenzao wanaowaza parefu hata 100yrs mbele tunaaza blah blah.
Mbona hatulalamikii Wazungu kuja kuchimba madini na kumiliki migodi, kuja kuchimba gas na mafuta pamoja na kumiliki vitalu baharini huko...
Huko baharini kuna visiwa tele havina watu vinazagaa zagaa na kuwa maficho ya pirates na wahuni wengine na wala husikii Tajiri dar es salaam hapo akitaka kununua na kufanya investment baadala yake wakija weupe tunaanza kelele nyiiingi..
Ni nani alishawahi kutoka na hela zake africa na kwenda kuwekeza kwenye ardhi ya USA au kununua kisiwa pale New Mexico au Kule Jersey akakataliwa?..