Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na hicho ndicho mnataka kitokee..."mtamezwa wabichi" ohoo.!!SGR na Stiglers ni White elephants
Wanangoja bwawa la Mwalimu Nyerere likamilike upatikane umeme usio wa jenerata ya Maharage yenye Makambakamba!Ujenzi wa reli hii ya kisasa kwa awamu ya kwanza kati ya Dar es salaam - Morogoro (Km 300), ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli Aprili 12, 2017. Ilielezwa ujenzi wa mradi huu ungekamilika ndani ya miezi 30 mpaka kufikia Novemba 2019, haikuwezekana.
Uliongezwa muda wa miezi 18 mpaka Aprili 2021, ikashindikana pia. Aliyekuwa waziri wa Ujenzi wakati huo, Leonard Chamuriho akaeleza reli hiyo ingeanza kufanya kazi ndani ya miezi minne, yaani Agosti 2021, ikashindikana tena.
Maelezo zaidi yakaonesha ingeanza kufanya kazi Disemba 2021, na waziri wa ujenzi na uchukuzi, Makame Mbarawa wakati akieleza mafanikio ya miaka 60 ya sekta ujenzi na uchukuzi.
Januari 17, 2022 Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa akaeleza awamu ya kwanza ya kipande cha Dar es Salaam-Morogoro utakamilika na majaribio yataanza April, 2022.
September 2022, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, alisema Treni ya umeme kutoka Dar es Salaam, hadi Morogoro itaanza kufanya kazi rasmi mwezi Februari 2023, kwani vichwa vya Treni, mabehewa ya abiria na mizigo yanatarajiwa kufika nchini mwezi Novemba.
Mei 2023, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilisema imepokea mabehewa sita ya reli ya kisasa ya (SGR) ambayo yamewasili kutoka nchini Ujerumani tayari kwa kuanza majaribio Juni 2023.
Kimya kizito mpaka sasa, kwani nini kinaendelea huko?