Aliyekuwa Dancer wa Wasafi chini ya Diamond Platnumz, Bajuni H. Bajuni ametangaza gafla kuachana na kazi iliyompa umaarufu ya kucheza mziki katika Shows na Video za mziki.
Ameandika kuwa leo ameamua kuachana na kazi hiyo ambayo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu toka utotoni na mpaka sasa amepita vingi kama dharau na mafanikio ndani yake, anaongezea kusema Umri sio rafiki, majukumu yanamuandama hivyo mwisho akatoa shukrani za dhati kwa mashabiki na kwa MUNGU. Na kuhitimisha hivyo.
Nahisi amepata hasira kuona Diamond ametajirika ila wao wanabaki vile vile na umaskini wao, wanaishia kupata hela ya kula na kodi tu ya kuishi vijumba vya kupanga