Dangote Anyakua 24.76% ya Kenya Pipeline kwa KSh bilioni 42.5, Aingia Zaidi Kwenye Biashara ya Mafuta Kenya

Dangote Anyakua 24.76% ya Kenya Pipeline kwa KSh bilioni 42.5, Aingia Zaidi Kwenye Biashara ya Mafuta Kenya

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote ameongeza uwekezaji wake nchini Kenya baada ya kupata 24.76% ya hisa za Kenya Pipeline Company (KPC) kwa takribani shilingi bilioni 42.5, hatua inayomfanya kuwa mwanahisa wa pili kwa ukubwa katika kampuni hiyo baada ya Serikali ya Kenya.

Ununuzi huo unakuja wiki chache baada ya Dangote kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu, mradi unaokadiriwa kugharimu takribani trilioni 2.1 na unaotarajiwa kuhudumia Kenya pamoja na masoko mengine ya Afrika Mashariki.

Sasa hisa hizo zimetoka wapi?
Dangote alipata hisa hizo kutoka kwa taasisi za Serikali na mifuko ya pensheni iliyokuwa imewekeza katika KPC wakati wa uuzaji wa hisa kwa umma (IPO). Taasisi hizo zilikuwa zimekusanya hisa nyingi wakati IPO ilipokaribia kushindwa kufikia kiwango cha fedha kilichohitajika. Chini ya miezi minane baadae, baadhi ya taasisi hizo ziliuza sehemu ya hisa zao kwa bei ya shilingi 9.02 kwa kila hisa. Muamala huo ulihusisha takribani hisa bilioni 4.5, zenye thamani ya bilioni 42.5.

Dangote sasa ana nafasi ya kushawishi maamuzi ya kimkakati ya kampuni hiyo, ingawa ushawishi wake halisi utategemea pia taratibu za utawala wa kampuni na maamuzi ya bodi.

Kwa nini KPC ni muhimu kwa Dangote?
Kenya Pipeline ina mtandao wa mabomba wa takribani kilomita 1,300 unaotumika kusafirisha petroli, dizeli na mafuta ya ndege kutoka Mombasa kwenda maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani, zikiwemo Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Dangote pia ametangaza mpango wa kuwekeza dola bilioni 1.5, sawa na takribani bilioni 195, katika upanuzi wa mtandao huo wa mabomba. Hii ni sehemu ya mkakati wake wa kuunganisha uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa mafuta katika masoko ya Afrika.

Ikiwa mipango hiyo itatekelezwa, Kenya inaweza kuwa kitovu muhimu zaidi cha usambazaji wa bidhaa za mafuta katika Afrika Mashariki. Hata hivyo, manufaa kwa watumiaji wa kawaida ikiwemo uwezekano wa kupungua kwa gharama za mafuta yatategemea utekelezaji wa miradi, ushindani sokoni na sera za Serikali.

Hatahivyo, muamala huu pia umeibua mjadala kuhusu sababu zilizofanya taasisi za Serikali kununua hisa nyingi wakati wa IPO, kisha kuuza sehemu yake miezi michache baadae.

Kwa Wananchi, maswali muhimu ni kama taasisi hizo zilipata thamani nzuri kwa fedha za umma, ni sababu zipi zilizosababisha kuuza hisa hizo, na mabadiliko ya umiliki yatakuwa na athari gani kwa kampuni inayosimamia miundombinu muhimu ya mafuta nchini.

Dangote sasa anawekeza katika kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu na amepata karibu robo ya hisa za Kenya Pipeline. Je, huu ni uwekezaji unaoweza kuimarisha nafasi ya Kenya katika biashara ya mafuta Afrika Mashariki au Serikali inapaswa kueleza zaidi kuhusu uuzaji wa hisa za taasisi za umma?
 

Attachments

  • 1980.jpeg
    1980.jpeg
    27.5 KB · Views: 9
Wakenya hongereni sisi huku tunaendelea kufanya tathmin ya elninyo
 
Back
Top Bottom