Dangote Cement penetrates giant Kenyan Cement Market

Viongozi waliposema tanzania ya viwanda walimaanisha viwanda vya wagonga nyundo kama sido. Sasa nyie mnawasuprise na likiwanda lenu kubwa hivyo unategemea nini. Lifungeni bana
Umenifanya nicheke bila kufungua kinywa maana sijaswaki bado.
Ningefungua kinywa mbu wangekufa.
 
UNA HEKIMA SANA . ..UBARIKIWE SANA . ........anaye chukia kwao MTUMWA
 
Viongozi waliposema tanzania ya viwanda walimaanisha viwanda vya wagonga nyundo kama sido. Sasa nyie mnawasuprise na likiwanda lenu kubwa hivyo unategemea nini. Lifungeni bana
Hata kàma ni nchi ya viwanda, kumbuka kwamba tunatakiwa kureview mikata yote, ili ikae kimaslahi zaidi, co kwa kuwa aliahidiwa kupewa gesi ya bure wakati huo, je cc ni kwa ajili ya kumnufaisha yy? kama hawezi andoke, na huko Kenya ndo alitaka kujenga hiki kiwanda kabla na baadae kuamua kukijenga hapa tz na kama pia kaamua kurudi Kenya bado sio mbaya, inawezekana ndo namna ya uwekezaji wake huo.
 
Hii ndio shida ya kuwapa watu uongozi wa mambo ya biashara wakati ajawai kumiliki kibanda cha kuuza nyanya.
 

Usiandike usichokijua,umesoma taarifa ya TPDC?
 
Watu mnapenda sana kuabudu wawekezaji. Yaani mnaona demand zao ni za msingi kuliko maslahi ya taifa. Haohao tena mnakuja kuanza kuponda kwamba serikali inaingia mikataba inayowanufaisha zaidi wawekezaji kuliko taifa. Hizi mindset za namna hii hazitalijenga taifa hata kidogo. Lazima tufike mahali tukubali kuweka maslahi ya taifa kwanza kuliko kukubaliana na kila anachokitaka mwekezaji. Tulishafanya makosa kwenye madini hatuwezi tena kurudia makosa kwa wawekezaji wapya eti kisa tu wataenda nchi jirani. Bora tubaki na umaskini wetu pamoja na natural resources zetu kuliko kushangilia umati wa wawekezaji wasiokuwa na faida pana kwa taifa.
 
Sawa.itakuwa hitilafu ya mitambo inekuwa kubwa.
 
Kuna uzi humu una sound clip ya mfanyakazi mmojawapo wa Dangote.
Maelezo yake yanaonesha serikali hii imekiuka makubaliano
Order za makaa ya mawe zinacheleshwa na tani hutolewa kidogo kidogo wakati kiwanda kinahitaji tani nyingi kwa wakati mmoja.
Ninaamini huo ndo ukweli maana waziri mmoja aliongea jambo kuhusu Dangote halafu siku iliyofuata akasema alificha baadhi ya taarifa(Dangote alitaka apewe gesi bure).
Kwangu huu ni uongo mkubwa.
Ametujicha mangapi?
Je, hajaficha habari zingine kweli?
Viongozi wa TZ wanasahau kuwa nyuma ya mwekezaji mmoja, kuna wawekezaji saba. Kushabikia mwekezaji mmoja kuondoka ni kushangilia na hao wengine kuondoka kwao.

Nagu alieleza kuwa lengo la kumleta Dangote ni kudhibiti mfumko wa bei ya saruji ambayo ilikuwa inapangwa na kikundi cha wazalishaji wa saruji. Dangote alitakiwa ajipangie bei yake (kutokana na uhalisia)
Watanzania ni mashahidi. Wengi tumejenga na saruji ya Dangote.
Iasemekana kuna fitina ya wazalishaji wa saruji ambao ni wahanga ktk ushindani wa soko la saruji. Ndo maana walishangilia sana ktk mkutano na waziri(ambao Dangote hakwenda) walipoambiwa wanatakiwa kununua makaa ya mawe nchini.
Kama sijaeleweka nisamehe mkuu maana hata mi sielewi hii movie.
Tafakari
 
Tanzania ya viwanda ni wimbo tu!! Hauna uhalisia hata kidogo
 
Kinachosikitisha ni kuona awamu ya nne ilijitolea kuandaa Katiba mpya, lakini wahafidhina wakampotosha kiongozi na kuleta Inayopendekezwa yenye mambo yaleyale ya kizamani. Ama kwa hakika Maoni ya Wananchi ambayo Jaji Warioba waliyakusanya, yalikua na mambo mazuri sana kwa mustakabali wa nchi, lakini looo, tumebaki palepale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…