Dangote lamu refinery: Mashine Tani 2,930 Zawasili, Ujenzi Waingia Hatua Mpya

Dangote lamu refinery: Mashine Tani 2,930 Zawasili, Ujenzi Waingia Hatua Mpya

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
Bandari ya Lamu leo imepokea meli ya MV Da Yang ikiwa na shehena ya metric tani 2,930 za mashine na vifaa vizito vinavyolengwa kutumika katika ujenzi wa Dangote East Africa Refinery. Meli hiyo inawasili siku chache tu kabla ya hafla ya uwekaji jiwe la msingi inayotarajiwa kufanyika Septemba 30, 2026.
571.jpg

573.jpg
572.jpg

Kuwasili kwa mzigo huo kunatoa ishara nyingine kwamba mradi wa shilingi trilioni 2.2 unaelekea kwenye hatua ya ujenzi, baada ya maandalizi ya awali ya eneo, usanifu na kazi za uhandisi.

Refinery hiyo inapangwa kuwa na uwezo wa kuchakata mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, na ikikamilika itakuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya kusafisha mafuta barani Afrika. Inatarajiwa kuhudumia Kenya pamoja na masoko ya kikanda.

Lakini Lamu Refinery si refinery pekee.
Serikali imeeleza kuwa mradi huo utakuwa sehemu ya mfumo mpana wa petrochemical na viwanda, ukiambatana na shughuli za nishati na uhifadhi. Aidha kuna mipango ya miundombinu inayounga mkono mradi huo, ikiwemo kituo cha kuzalisha umeme cha megawati 1000.

Je, Lamu iko tayari kwa mabadiliko haya makubwa ya kiuchumi na miundombinu ambayo refinery hii na miradi yake inayohusiana inaweza kuleta?
 
Back
Top Bottom