Hivi Pascal unaona haya mambo kama ninavyoyaona, kuangalia hili suala beyong the pernonality of Dangote? Samia anaingia katika haya majadiriano katika context ya personal goodwill na Dangote. That is very wrong.
Dangote amekaribisha ubia na Tanzania kujenga refinery MOMBASA. Hivi Samia ameelewa hilo?
Hii ni invitation sawa tu na ile waliyopewa Uganda, Rwanda, South Sudan, DRC. Kwa kifupi, Dangote anataka kujenga Refinery kwa kutumia hela za hizi nchi, na wakati huohuo anajifanya anatufanyia favor. Kama tunakuwa partners, kwa nini iwe na Dangote? Why not any other preferred investor?
Samia alipaswa kumuuliza Dangote kwa nini wewe na sio Dewji kwa mfano? Kwa nini isiwe tajiri mwingine wa Afrika?
Samia anapaswa kuelewa Dangote anataka kututumia kujenga monopoly ya refinery Africa. Dangote akiwa na Refinery mbili kubwa Africa then anakuwa monopoly, hana mshindani na itafikia anawaamrisha anavyotaka. Tutapoteza energy security kwa kuwa under his mercy.
Ushauri wangu kwa kina Samia ni kwamba, kwa kuwa Dangote ana refinery kubwa Nigeria, hapaswi kuruhusiwa kujenga refinery East Africa, au popote Africa. Kama Refinery itajengwa East Africa au kwingineko Africa basi ijengwe kwa namna ya kuleta ushindani na Refinery ya Dangote.
Tunahitaji refinery sana, lakini isiwe by Dangote.
Na pia waelewe Dangote ni mortal man, kuna wakati hatakuwapo na hujui nani atakuwa na share zake, na atakuwa mtu wa namna gani. Inaweza kuwa kampuni ya nje ambayo nia yake ni profit tu. Sasa wasijiingize kwenye hii kitu kama Dangote ni mjomba wao atakaeishi milele. Inawezekana kuna siku Dangote akawa hana nguvu ya umiliki wa hizi refineries. Atakaekuwa na umiliki mkubwa atatufanya sisi watumwa wake.
Kwa nini hawa watu hawaoni ujanja huu wa Dangote bali wanamwona kama Msamaria mwema?