Dann Sserenkuma kuvunja mkataba na Simba SC, Uchawi watajwa kuwa sababu

Dann Sserenkuma kuvunja mkataba na Simba SC, Uchawi watajwa kuwa sababu

Hivi huwa mnapata faida gani kuandika habari za kutunga na za uongo kama hizi? Ingekuwa ni kwenye gazeti tungesema labda ulikosa habari ukaamua uandike tu ili kurasa zijae.

Hii habari ya kukatisha mkataba imeandikwa kwenye gazeti la Mwanaspoti na sababu kubwa imeelezwa ni kulinda kipaji chake kwa sababu amekuwa hachezeshwi mara kwa mara sasa hizo sababu za kwamba timu haina mwendelezo mzuri na sijui ni kwa sababu ya ushirikina mara wenzake wanamchawia wewe umezipata wapi?

Mara nyingi tunapenda sana kulaumu waandishi wa habari kwa kupenda kuongeza chumvi kwenye habari zao lakini huwa tunalazimika kuwaelewa kwamba labda hawajasoma vizuri ndo maana wanafanya hivyo au kwa sababu wanajua wateja wao wanataka nini hivyo wanapenda kuongeza chumvi ili wafanye biashara, sasa wewe kuongeza chumvi, tena hii sio chumvi tuseme ni kuweka sumu kabisa nini msukumo wake?

Upinzani wa jadi sio lazima uandike mabaya kwa mwenzako hasa yale ambayo sio ya kweli.

😕
 
Attachments

  • 1426802187549.jpg
    1426802187549.jpg
    68 KB · Views: 222
Timu ambayo inamlipa mchezaji wake Okwi 5.3m kwa mwezi, unasemaje "kuna njaa"?
Timu ambayo juzi juzi ilmkabidhi 80m mkude na kudouble mshahara wake, huoni aibu kusema "kuna njaa"?
Timu ambayo inaendelea kumlipa kiongera mshahara mnono japo imemuondoa katka list ya wachezaji iliyowasajili, unapataja wapi nguvu ya kusema "kuna njaa"?
Timu ambayo ilitumia zaidi ya 80m kuvuka bahari ya hindi kwenda kujiandaa na mechi ya Yanga, huoni soni kusema "kuna njaa"?

Labda sijui maana ya neno "kuna njaa".

Mlienda kuua Albino ili tu muwafunge Yanga Fc... Kuwa mkweli tu mkuu.
 
Timu ambayo inamlipa mchezaji wake Okwi 5.3m kwa mwezi, unasemaje "kuna njaa"?
Timu ambayo juzi juzi ilmkabidhi 80m mkude na kudouble mshahara wake, huoni aibu kusema "kuna njaa"?
Timu ambayo inaendelea kumlipa kiongera mshahara mnono japo imemuondoa katka list ya wachezaji iliyowasajili, unapataja wapi nguvu ya kusema "kuna njaa"?
Timu ambayo ilitumia zaidi ya 80m kuvuka bahari ya hindi kwenda kujiandaa na mechi ya Yanga, huoni soni kusema "kuna njaa"?

Labda sijui maana ya neno "kuna njaa".

Wewe hata timu yako huijui vizuri, Mkude alidai 80m akapewa 25m na gari naskia kaenda kudai hela iliyobaki akaambiwa thamani ya gari ni 60m. kiongera lazima alipwe kwani angefungua kesi kama Musoti . Unajua Tambwe bado anawadai hela za kuvunja mkataba?
 
Kama huwalipi vizuri na kwa wakati wachezaji wako watalipwa na maadui zako.
 
Wewe hata timu yako huijui vizuri, Mkude alidai 80m akapewa 25m na gari naskia kaenda kudai hela iliyobaki akaambiwa thamani ya gari ni 60m. kiongera lazima alipwe kwani angefungua kesi kama Musoti . Unajua Tambwe bado anawadai hela za kuvunja mkataba?

Jonas Mkude aliposaini mwaka jana, alipewa 80m, Toyota GX 115 na mshahara wake ukapaa hadi 2m.

Baada ya kuona ameondolewa kikosini, Kiongera aliomba aachwe ili atafute timu nyingine ili "kulinda kipaji chake". Simba Sc "Taifa Kubwa" waligoma kumuacha, ila waliamua kumpeleka kwa mkopo ligi ya Kenya.. na mshahara wake wanamlipa kama kawa.

Mkataba wa Tambwe na Simba Sc unaujua vizuri? Kama Tambwe anaidai Simba Sc kwanini asiwashitaki TFF, FIFA au hata CAS? Kila siku amekalia kupiga domo tu.. mara "simba nawadai".. mara "sijui hata hela zangu nitazipataje"..
Tambwe hadai chochote Simba Sc.
 
mkuu watafsirie kiswahili unajua mashabiki wa simba wengi vilaza wa kingereza ona umebandika hili bado mtu anabisha mns ajaelewa kilichoandikwa wakiitaji kirusi nijuze niwatafusirie
 
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Dann Sserenkuma aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya ameomba viongozi wa Simba kuvunja mkataba nae.

Dann bado hajarudi kutoka kwao, aliomba ruhusa kuwa ana matatizo ya kifamilia, alitakiwa awe amerudi toka wiki iliyopita lakini ametuma taarifa ya kutaka kuvunja mkataba.

Kanuni za simba zinaruhusu kufanyika mazungumzo ya uvunjaji mkataba, endapo Mchezaji hajaonyesha kiwango kizuri cha kusaidia timu.

Chanzo cha ndani kinaeleza baadhi ya sababu kuwa kichochezi kwa kuondoka kwa mchezaji huyo.

1. Kukaa Benchi muda mrefu bila kucheza.
2. Timu kutokuwa na muendelezo mzuri kwenye Ligi.
3. Pia Sserenkuma alieleza zaidi kuwa baadhi ya Viongozi wa Simba SC wanamlazimisha kutumia madawa ya ushirikina ( kwa mfano: ya kupata na kuogea) ili kuiwezesha simba ifanye vizuri katika mechi A ligi Kuu.

Danny Sserenkuma ameonekana akikerwa na imani ya Club ya simba katika masuala ya ushirikina.

Anasema kuna baadhi ya wachezaji wenzake wana mchawia kiwango chake ili waweze pata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Si ajabu hicho chanzo cha ndani ni ubongo wako
 
Mtasema yote nyie ila Ipo Siku utaipenda Simba mnyama Taifa kubwa tuachien Simba yetu

Siku ambayo serikali ya Tanzania itaruhusu waganga kufanya kazi zao hadharani.

Timu imejaa wachawi.
 
Back
Top Bottom