DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Me kitu ambacho huwa nashindwa kuelewa ni pale tu tunapojuzwa alfa lkn omega hatuambiwi kuwa imeaMriwa vp
Mkuu mbona kwenye issue ya Lugumi tulijuzwa Omega?
Waziri alisema kua Lugumi alikua Sahihi kabisa ila Serikali ndo ilikosea.
 
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

View attachment 917003

Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.

View attachment 917001
View attachment 917002

Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums

===========
Mfanyabiashara Akram Azizi amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 9,018.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 70 ya kukutwa na silaha, mawili ya kukutwa na risasi, mawili ya kukutwa na nyaraka na moja la utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali wakuu, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana. Mshtakiwa ameenda rumande katika gereza la Segerea.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2018.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mtanikumbuka. Wazee hata mimi Pogba namkumbuka. Kuna ushenzi asingeukalia kimya.
 
Mtanikumbuka. Wazee hata mimi Pogba namkumbuka. Kuna ushenzi asingeukalia kimya.
Alikuwa tapeli tuu mwendazake alijaa visasi,je ilivoisha uliona? Alifanya vile akilenga jambo baada tu la kulipata wakamuachia
Alichokua anakifanya ndicho vijana wake akina sabaya walikua wanakifanya
 
None sense kabisa
Kwani lazima anitapeli mimi?
Aliyekuambia mtu kuwa tapeli npaka akutapeli wewe ni nani?
Na muaji lazima akuue wewe?
Waliotendewa sio binadamu kama wewe?

Kwahiyo nikubali tu bila kujua amemtapeli nani? Natural justice haifanyi kazi hivyo.
Na haina maana namtetea. Labda kweli ni tapeli
 
Kwahiyo nikubali tu bila kujua amemtapeli nani? Natural justice haifanyi kazi hivyo.
Na haina maana namtetea. Labda kweli ni tapeli
Ungetaka kujua kamtapeli nani basi swali lako ingekuja hivyo,sasa wewe umeniuliza mm kwamba amekutapeii nini?
Umeonyesha kichwa chako ni empty kabisa
Mtu kuitwa tapeli umemaanisha mpaka akutapeli wewe,ingekuwa hivyo pasingekuwepo mkosaji maana ata hakimu angesubiri mpaka atapeliwe yeye ndo aamini kweli utapeli,udhurumaji,wizi n.k upo kwa kuwa yeye kafanyiwa
Kinyume na hapo hapana
Anyway ngoja tuache maana Tunayemuonge
a alishazikwa
 
Watanzania bwana...tunapenda kutunga maneno maneno bila ushahidi. Kutwa umbeya.
Sibithisha amemtapeli nani. Usiseme tu kama wote tuko kwenye msafara wa nyumbu tunavuka Serengeti
 
Back
Top Bottom