Dar: Barabara ya Jangwani yafungwa kutokana na mvua zinazoendelea

Dar: Barabara ya Jangwani yafungwa kutokana na mvua zinazoendelea

HIYO NDIO HALI YA DARAJA LA MTO MSIMBAZI MJINI DARES-SALAAM LEO LIMEFURIKA KWA MAJI HAPAPITIKI NA KUNA VIONGOZI WA SERIKALI WANAO HUSIKA WAHESHIMIWA MKUU WA MKOA, MBUNGE NA WAZIRI ANAYE HUSIKA WAMEYAFUMBIA MACHO HAYO MAJANGAA YA MAJI, UTAFIKIRI HAWAYAONI MADHARA YANAYO WAKUTA WATU WA MAENEO HAYO NI HATARI SANA KWA USALAMA WAO KIMAISHA.
View attachment 1396435




Bar_she_te si alisema atajenga daraja hapo la 300m kwenda juu?
 
Serikali ya ccm ilishakataza. Kuzusha mambo kama wale wa arusha
Mbona watu hawaelewi?
Kuna cha kuzusha mambo hapo?au Ukisema ukweli una ambiwa umezusha mambo? Au mpaka wafe watu ndio utajuwa kuwa hayo maji yanayo madhara kwa binadamu?Kaka unazeeka vibaya nini?
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa unajipenda kweli kuripoti jambo kama hili kwa serikali hii inayojipambanua kuweka miundo mbinu bora kabisa kuliko awamu yeyote?
Kwani ni kweli huyo ni mwenyekiti wa mtaa?
 
HIYO NDIO HALI YA DARAJA LA MTO MSIMBAZI MJINI DARES-SALAAM LEO LIMEFURIKA KWA MAJI HAPAPITIKI NA KUNA VIONGOZI WA SERIKALI WANAO HUSIKA WAHESHIMIWA MKUU WA MKOA, MBUNGE NA WAZIRI ANAYE HUSIKA WAMEYAFUMBIA MACHO HAYO MAJANGAA YA MAJI, UTAFIKIRI HAWAYAONI MADHARA YANAYO WAKUTA WATU WA MAENEO HAYO NI HATARI SANA KWA USALAMA WAO KIMAISHA.
View attachment 1396435

Waziri wa afya anasema kuzuia corona tunawe mikono na sabuni kwa kutumia maji tiririka, haya si maji tiririka? Neno safi ameliacha wapi?
 
Kipindi DART wanajenga zile ofisi Magu alikuwa na cheo kipi serikalini ?
waziri wa ujenzi!
ila kuna mengi aye alikuwa anaoperate under some one
pale jangwani ni mkusanyiko wa mambo mengi yaliyiokosewa tangu huko nyuma ujenzi holela - mipango miji . hivyo kuondoa uata ni kuweka daraja la juu kuanzia magomeni kwenda mpaka fire
 
Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 10:15 jioni kutokana na mafuriko kwa mvua inayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam

Wasafiri wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara. Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji

Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, tunawashauri kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo na sehemu nyingine za Jiji

ZINGATIA: Nawa mikono kabla ya kuingia kwenye Basi, Panga foleni ukiwa kituoni kwa kuingia kwenye Basi, Usiingie kwenye Basi kwa kugombania, Subiri Basi linalofuata endapo Basi iliyopo imejaa, Bila kunawa mikono kwa sabuni au dawa, hautaruhusiwa kuingia kwenye Basi
Je wakati wa kutoka kuna kunawa mikono? Vile viti na mkanda ya kushika vyote hutumiwa na watu wengi na hivyo unaweza kuwabeba hao Corona na kuwaambukiza watu wengine.
 
Back
Top Bottom