Dar: Bodaboda kupatiwa namba maalumu ili kuongeza usalama

Dar: Bodaboda kupatiwa namba maalumu ili kuongeza usalama

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza mchakato wa kuboresha sekta ya usafiri wa bodaboda kwa kusajili madereva, kuwapatia namba za utambulisho, vituo rasmi vya kuegesha, na mavazi yatakayoongeza imani na usalama wa huduma wanazotoa.

Akizungumza katika kongamano maalum la maombi na dua kwa madereva wa bodaboda na bajaji, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mpogolo amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo katika uchumi wa miji na usafiri wa kila siku. Ameeleza kuwa hatua hizo ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha huduma za usafiri wa bodaboda zinakuwa salama, nadhifu, na zinazoaminika zaidi kwa wananchi.

Katika kongamano hilo, Mpogolo ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda amani ya taifa, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 
Si wote ila kuna vibaka wengi wanaojificha kwenye boda, nice move.
 
Ni suala tu la muda kabla hawajaanza kulipa kodi na tozo mbalimbali. Maana yule Rais wao wa wanyonge hayupo tena! Hivyo kwa sasa kila mtu apambane na hali yake.
 
Hawa wahuni bora kuwadhibiti.

Maana ni wapumbavu waliopitiliza.
 
Back
Top Bottom