Dar Derby: Polisi takribani 550 kuimarisha ulinzi uwanja wa taifa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni katika pambano la Simba na Yanga ambapo wanasiasa na viongozi wengi wa kisiasa wanatarajiwa kuhudhuria. Msemaji wa TFF amesema kutakuwa na askari wenye sare 400, askari kanzu 150, vikosi vya mbwa na farasi. Alfred Lucas amewakaribisha wapenzi wote wa michezo kushuhudia pambano hilo. Source EATV habari!
 
hao badala ya kuangalia usalama watakuwa wanaangalia mpira....
ni hasara tupu hiyo
 
Uwanja mdogo.......saa 9 utasikia milango imefungwa wa ndani wa ndani........kero umefun safari yote kutaingia...mwengi tubakie kwa runinga !!
 
Haya sasa RAIA kazi kwenu wanajileta wenyewe uwanjani zamu yenu kuwapa kipigo nafikiri kwamba mtawamudu hao wahuni
 
550 katika uwanja wa watu 22,000/-

Kwa hesabu za haraka askari mmoja atakuwa anaangalia mashabiki 44.

Sioni haja ya kuwa na askari wengi kiasi hicho labda kama kuna taarifa za kiintelejensia zinazoshawishi matumizi ya askari wote hao.
 
Wote hawa kwani kuna viti vya kung'olewa pale
 
550 katika uwanja wa watu 22,000/-

Kwa hesabu za haraka askari mmoja atakuwa anaangalia mashabiki 40

Sioni haja ya kuwa na askari wengi kiasi hicho labda kama kuna taarifa za kiintelejensia zinazoshawishi matumizi ya askari wote hao.
 
Kesho mitaani hakuna ulinzi kwa mpango huo.
Hii ni zaidi ya kuzuia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA.
 
Watakuwa wamenusa viashiria vyenye picha ya siasa. Mechi ya mwisho kulikiwa na taarifa za kiintelijensia kwamba kulikuwa na watu walipanga kutoa jumbe za kisiasa pamoja na kuchoma kadi za chama fulani. Sasa hivi nchi ipo kwenye tension ya kisiasa, wasije watu wakaja na Tshirt zenye picha ya mwanasiasa au kuanza kuimba au kufanya lolote kuonesha mrengo wa kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…