Nikiwa kwenye mizunguko yangu, nilipata nafasi ya kutembelea eneo la Kawe katika Viwanja vya Tanganyika Packers, ambako kumekuwa na shughuli mbalimbali zikiendelea hapo ikiwemo zile za masuala ya ibada mfano Kanisa la Mwamposa ambalo limekuwa likiendesha ibada zake hapo mara kwa mara.
Kanisa hilo limekuwa maarufu kutokana na wingi wa Waumini wanaohudhuria ibada zake kila wiki.
Hata hivyo, hali ya mazingira ya eneo hili inazua maswali mengi na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa afya za waumini na jamii inayozunguka eneo hilo.
Uchafuzi wa Mazingira na Ukosefu wa Vyoo
Kanisa hili linapokea waumini wengi wa rika mbalimbali kila Jumapili na siku za ibada maalum. Hata hivyo, changamoto kubwa ni ukosefu wa vyoo vya kutosha vinavyoweza kuhudumia idadi hii kubwa ya watu.
Vyoo vilivyopo ni vichache na viko ndani ya kanisa, hali inayofanya waumini wengi kushindwa kupata huduma za msingi kwa wakati inapotokea kuna shughuli za ibada zinaendelea hapo.
Kutokana na uhaba wa vyoo, baadhi ya Waumini wanalazimika kujisaidia pembeni ya uzio unaozunguka Viwanja vya Kanisa.
Matokeo yake, eneo hilo limejaa harufu kali ya mikojo na kinyesi, na virundo vidogo vya uchafu vinaonekana kila mahali. Hali hii sio tu inaharibu taswira ya eneo hilo, bali pia inahatarisha afya za waumini na wapita njia.
Maoni ya Wakazi wa Eneo Hilo
Nilipozungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo, hasa wajasiriamali ambao hufanyabiashara katika viwanja hivyo, walielezea kero kubwa wanayokumbana nayo.
Walisema harufu mbaya na uchafu unaozagaa eneo hilo unaathiri biashara zao, lakini wanalazimika kuvumilia kwa sababu ya wingi wa waumini ambao ni wateja wao wa kudumu.
Wananchi hao walisema wamejaribu kupeleka malalamiko yao kwa viongozi wa serikali za mitaa na halmashauri ili hatua zichukuliwe, lakini juhudi zao zimezaa matokeo kidogo.
Kwa mujibu wa maelezo yao, juhudi za awali za kusafisha eneo hilo hazijakuwa za kudumu, na changamoto hiyo bado inasumbua sana.
Hatua za Uongozi
Kwa kuwa nilitaka kupata picha halisi ya hatua zilizochukuliwa, nilizungumza na Katibu wa mazingira Kawe pamoja ambaye ndio anayehusika na mazingira.
Alieleza kuwa suala la uchafu katika viwanja hivyo limejadiliwa mara nyingi na hatua kadhaa zimechukuliwa, ikiwemo kuhimiza waumini kuacha kulala katika viwanja hivyo baada ya ibada.
Hata hivyo, walikiri kuwa changamoto hiyo ni kubwa na bado haijapatiwa suluhisho la kudumu.
Walisema masuala ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa yameathiri kasi ya kutatua tatizo hilo, lakini wameahidi kulijadili upya baada ya uchaguzi ili kuona namna bora ya kulishughulikia.
Mapendekezo na Wito
Viongozi na waumini wa kanisa hili, wamekiri kushuhudia mara kadhaa usafi ukifanyika ndani ya kanisa pekee, huku eneo la nje likiachwa katika hali mbaya.
Mimi kama muumini wa kanisa hilo sinabudi kusema, juhudi za kuhakikisha usafi unafanyika katika maeneo yote, zinahitajika sana ili kulinda afya za waumini na wakazi wa eneo hili.
Kwa kuwa kanisa linajivunia idadi kubwa ya waumini, ingekuwa vyema kama lingetenga rasilimali kwa ajili ya kuboresha huduma za msingi kama vyoo na usafi wa mazingira kwa ujumla.
Pia, mamlaka za halmashauri na viongozi wa eneo hili wanapaswa kushirikiana kwa karibu na uongozi wa kanisa ili kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa kwa haraka.
Nihitimishe Kwa kusema, mazingira safi na salama ni haki ya kila mmoja wetu.
Ningependa kutoa wito kwa uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kuchukua hatua za dharura kushughulikia tatizo hili, kwani afya za waumini na wakazi wa eneo hili zinaendelea kuwa hatarini kila siku.
Tunapaswa kushirikiana kuhakikisha kuwa ibada zetu zinafanyika katika mazingira yanayoheshimu utu na usalama wa kila mmoja.