carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkoa wa Dar es Salaam umedhamiria kufanya kampeni ya kupita nyumba kwa nyumba kuandikisha bima ya afya kwa wote.
Hilo limesemwa leo Alhamisi Oktoba 23, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alipokuwa alizindua awamu ya pili ya kuandikisha wa bima kwa wote awamu ya pili inayozindulia nchini kote.
Kifurushi cha huduma hii ni mpango wa utekelezaji wa Sheria Bima ya Afya kwa wote sura 161 unaowezesha wananchi kuchangia huduma za matibabu kabla ya kuugua ili kuwa na uhakika wa matibabu watakapougua ambapo kila Kaya itapaswa kuchangia Sh150,00 kwa mwaka kwa ajili ya watu sita.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mnazimoja, Chalamila amesema shughuli hiyo wataifanya kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya na taasisi binafsi lengo likiwa kuhakikisha kila mkazi wa mji huo anakuwa na bima.
Chalamila amesisitiza kuwa jambo hilo sio Siasa na kuwaomba wakazi wa Mkoa huo wanapojiunga na bima hiyo kuonana kama wamepoteza hela yao na faida yake watakuja kuiona baadaye.
Chanzo :Mwananchi official