NINAPOITAZAMA TANZANIA YANGU, NAPATA MASWALI MAGUMU SANA!
Hivi unategemea nini kwa jiji kama Dar es Salaam, lenye miundombinu ile ile aliyoacha Nyerere hata kama tutaongeza magorofa jiji zima?????
1. Kama umeme wa kariakoo ulipimwa kusambazwa kwa nyumba mia moja...sasa hivi kuna magorofa labda mfano kumi na kila ghorofa lina vyumba 20...unategemea nini kuhusu huo umeme? we jaribu kuwauliza hao wanaojenga maghorofa hivi wanategemea kuvuta umeme huu huu au kuongezewa gridi yao??? is that how you call planning?
2. Kama kampuni ya maji inasambaza lita zile zile za maji tangu ukoloni...na magorofa yanaongezeka...wategemea nini? we fikiria drainage system ya magorofa yanayojengwa huko posta itakuaje? na wanategemea maji kwa kuchimba visima au dawasa???
3. Angalia barabara ya kariakoo iko tangu enzi za mkoloni hadi leo...no 'update'??
Poor Tanzania!
Mkuu bongo ovyo, ndio maana huwa tunajiuliza, hivi hao wanaojiita city council, mayors na wabunge wa dar pia huwa wanajaribu hata kutjitokeza mbele za watui na kusema sisi ni viongozi wa dar? angalia picha ya dar kutokea juu, kwa watu wenye akili ukubwa wa dar na pamoja na idadai ya watu wake kule uwanja wa ndege, tabata, mbezi hadi huko kibamba, ilitakiwa bado iwe msitu kabisaa, lakini watu walivyo ovyo kwa mipango, hayo maeneo yote yameharibiwa ni vurugu tupu, hata kama ukajenga nyumba nzuri ya kifahari huko, jiandae baada ya miaka mitatu minne hapatakuwa tofauti na mchikichini, kwa kuwa mtu ananunua kiwanja cha kuweza kujenga nyumba moja, halafu yeye atakigawa mpaka zitapatikana nyumba hata kumi, sasa hapo unategemea nini hata kama wamepima viwanja vizuri? eneo la ilala, vingunguti , tabata bima, lingeweza kujengwa nymba ambazo zitawakusanya watu wengi katika eneo moja, na kuwahudumia kwa mahitaji yote, usafiri, maji, posta umeme, nk, hivyo lingecontrol watu kusambaa hadi huko gongolamboto, mchikichini, magomeni, likijengwa na kupangwa vizuri linaweza kufyonza watu wote waliosambaa hadi huko mwenge na maeneo mengine, nyumba za kawaida au ngorofa kadhaa kila moja yenye uwezo wa kuwa hata na units 50 au hata 30, zingeweza kutumia vizuri maliasili ya ardhi tuliyonayo na hata hatungekuwa na hii migogoro, keko , kurasini ingefyonza watu wote hata mbagala sasa hivi ingekua bado pori, akini sasa hivi nenda mbagala ukiangalia watu wanavyosambaa ni aibu, itakua kasheshe katika kuwahudumia watu hawa, na hata kuwapatia ulinzi itakua kazi, ardhi ya dar inachezewa tuu, na aibu kwa hao wanaojiita wazee wa jiji, wanachezea nchi yetu, na kutuaibisha tuu, dar katikati bado kupo empty sana, wakiweka miundombinu inayostahili ya maji safi na taka na kupanua barabara kidogo au kulimit idadi ya magari yanayoingia kule bado kuan uweza wa kujenga majengo mengo tuuu hata ya ghorofa 70 pale katikakti ya jiji, jengo la posta mpya ni uchafu tuu ule pale, wavunje wajenge jengo refu, pale ni uso wa jiji ladar na niuso wa tanzania kwani ni jiji kubwa na ni center ya kila kitu, uchumi utamaduni nk, sasa kama pale kupo vile kwingine si aibu tuu, kiapnde cha ardhi kutoka ferry soko la samaki mpka kwney kituo cha boti za zanzibar pia wamechezea, hilo eneo linaweza kupanuliwa zikajengwa barabara pana na kuhamisha misongamano katikati ya babarabara za mji na wanaweza kujenga maeneo mazuri ya kupumzikia watu, hebu angalia watu wa dar wana eneo gani la public la kupumzikia? manazi mmoja ndio kufuli kila siku, hilo eneo lingepiwa marumaru na maeneo ya nyasi yakao machache pembeni pamoja na miti na maua, lakini wakiacha vile na majani watu watapitapita na majani yatakanywagwa na kuacha njia nyingi kama za panya, halafyu vumbi pia, kudadadeki, bongo bado, labda kwa sababu nchi yetu ni masikini, inaona haiwezi kufanyia dar mambo hayao wakati watu wengine nchini hawana hata hospitali, au hata madarasa, kuna chuo cha ardhi tanzania, sijui wanasoma nini? au bado hawajafundihwa chochote kuhusu urbanization, najua wenzetu mambo ya urbanization yalianza mika ya nyuma kule, hata wa uchumi hakuna anayesoma urban economy? wa utalii je? hivi bongo si tunasomaga kujibu maswali tuu ya mtihani? kuaply f, au ndio tuna matatizo gani?BTW, ingekuwa vizuri ukikutana na anayehusika na mambo haya , mfano meyor, kuna meya wa ilala ni kijanaaaa, na ana furaha muda wote, city council, wenyewe business wanayoiweza ni kunyanganyana maandazi na vitunguu kariakoo, wenyewe hiyo ndio wanaona ni kore business yao, kudadadeki, unaweza kukasirika mpka ukalipuka, na hakuna kinachifanyika, kwa huyo twigwa mzembe tanesco, at least kuna kitu kinafanyika, jiji sina uhakika, nina hamu ya kujua pia