Yafaa kujenga miji mipya nje ya jiji la Dar es Salaam kwa kuanzisha, new business centres. Maeneo ya Posta yaachwe kwa ajili ya ofisi za serikali. Kama yanaanzishwa maeneo mapya na huduma za kijamii zinafikishwa watu watasogea kufuata huduma za kijamii. Maeneo ya Tuangoma kumepimwa nafikiri tangu mwishoni mwa miaka ya 90, watu wamenunua viwanja, na wamejitahidi sana kujenga, lakini bado kasi ya watu kuhamia kule ni ndogo kwa kuwa huduma za kijamii kama vile umeme na maji havijasambazwa katika kiwango cha kuridhisha au hazijasambazwa kabisa.