Jiji limekuwa sana hasa kwa population, population density, wasiokuwa na kazi wengi sana, madalali (wavivu) wanaotaka mambo ya haraharaka bila kusota. Mimi napendekeza badala ya kukazania tu Dar tuimarishe miji mingine pia tu plan barabara vizuri na miundombinu mingine. Tusije tukafanya makosa tuliyofanya Dar. Ukiangalia kwenye picha linavutia sana na jiji litakudanga kwa kuonekana bomba sana lakini ukishuka, shuruba zilizopo ambazo zinatokana na kutokuwa surveyed na watu kujenga kiholela utakimbia. Pia hatujakaa poa kabisa sababu percentage kubwa sana ya pato inatoka hapa Dar. Hiyo haijatulia kabisa cha msingi ni kusambaza huduma za msingi na kuweka miundo mbinu ya kutosha kwenye miji mingine mikubwa angalau kuwe na miji kama mi nne au mitano ya watu kukimbilia huko, sio Dar Dar Dar tu. Dar itabaki kubwa sababu ya bandari, na biashara lakini sio ndio iwe kila kitu kama tunavyodanganyika sasa hivi. Mfano mzuri ni wenzetu wa Kenya angalia Mombasa, Nairobi na miji mingine inavyokuja juu.