ni vema sasa mamlaka zinazohusika zikaelekeza nguvu ya kuanzisha satellite towns pembezoni mwa jiji kuliko kung'ang'ania kuangusha maghorofa katikati ya jiji sehemu ambazo miundo mbinu ni mibovu kama vile barabara nyembamba, hakuna parking za kutosha, mifereji ya maji machafu inayoziba mara kwa mara n.k.Hizi satellite towns zitakuwa planned well kimiundombinu kulingana na hali halisi ya sasa na pengine hata ya miaka karibu hamsini ijayo.Hii pia itapunguza mlolongo wa watu wengi kufuata huduma katikati ya jiji kwa sababu miji hii mipya ya pembeni angalau itakuwa na maofisi mengi ya serikali, mashirika ya umma, biashara,elimu n.k.mfano mzuri ni mpango wa kuanzisha mji mpya wa kigamboni ingawa nao uanzishwaji wake umejaa changamoto nyingi.:target: