Haya ni maendeleo yana gharama zake nazo ni kama miundombinu mibovu kwa jiji linalokua kama Dar,WAKENYA WANADAI NAIROBI NDIYO JIJI KUBWA EAST AFRICA HATA KATIKA MTANDAO WANAJITAMBULISHA HIVYO NISAIDIENI KWA WALE WALIOFIKA NAIROBI HAYA MANENO NI YA KWELI?.
MBONA MIMI NILIFIKA NA KUKAA MWEZI MZIMA NA NILIBAHATIKA KUUTEMBEA MJI WOTE KWA MIGUU,JE HII INAWEZEKANA KWA DAR?.NAMNA GANI TUWAJULISHE HAWA WENZETU WASIENDELEE KUJIGAMBA HIVYO.
UKWELI JIJI LA DAR NI KUBWA SANA NAIROBI INAINGIA MARA 2.
Nairobi wana majengo marefu kadhaa, ambayo DAR bado haina, lakini baada ya miaka mitano Dar itakua na majengo marufu kibao na ya kisasa kulinganisha na ya NAIROBI ambayo mengi ni ya muda mrefu, mfano times tower ghorofa 38, ndio jengo refu kuliko yote AFRICA MASHARIKI NA KATI, ila halina muda mrefu kabla halijakua replaced na jengo ambalo lina ghrofa zaaidi ya 56 addis ababa, kuna majengo pacha ghorofa 35 yanajengwa sasa hivi jijini dar karibu na JM MALL barabara ya sokoine, na lingine lenye ghorofa 30 linaitwa RITA TOWERS, litabadilisha jiji la Dar kwa ujumla, Dar ni kubwa na ina matatizo ya foleni.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara wenzetu wako mbele yetu, sis bado tunazungmzia flyovers wenyewe washaanza kujenga na zitakamilika muda si mrefu, nadhani kuna barabara muhimu wanaita THIKA HIGHWAY KM 14 kama sijakosea, kwa jiji la Dar kazi imekwisha anza kujenga 21km za MABASI YAENDAYO KASI (BRT)na ndhani kwa hapotutakua na usafiri wa kisasa EAST AFRICA NZIMA.
Pia Dar tuna tatizo la umeme, sijui Nairobi hali ikoje, na kingine, muda si mrefu DAR itai-challenge Nairobi, pamoja na kuwa wao wanapanuka pia maeneo ya westland na upperhill, Tanzania itajenga jengo la gorofa kama 25 hivi pale upperhill Nairobi, pia katika maeneo ya jiji la Dar maeneo ya Upanga, Masaki, Kijitonyama na Mikocheni yanakua haraka pia kwa majengo mazuri na marefu ya makazi, Kariakoo ndo usiseme nasikia ishajaa.