Kutokana na mvua kuendelea kunyesha mara kwa mara Jijini Dar es Salaam hali ya usafi katika Soko la Kawe imekuwa siyo nzuri, mazingira haya yanatajwa kuwa sio salama kwa watumiaji sokoni hapo na wakazi wa maeneo ya Kawe.
Soko hilo lipo katika Jimbo la Kawe ambalo Mbunge wake ni Joseph Gwajima licha ya ushuru kukusanywa sokoni hapo lakini lipo hatarini kusababisha magonjwa ya mlipuko.