Dar es Salaam here I come naomba mnipokee waugwana!

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
3,988
Reaction score
1,308
Asalam alaikum wanajamvi, Namshukuru Mungu kwa kuiona siku mpya nikiwa na siha na afya njema. Baada ya kufika Tanga kuwaona jamaa na marafiki na sio kurenuu konsensa kama alivyosema "drphone" hatimae leo nipo njia moja narudi zangu Dar es Salaam.

Nimefungashiwa na wenyeji wangu pakacha la embe viringe, nazi, ndizi za bokoboko,halwa, vitoria,heltho ya lita 5 na vingine vingi. Japo kuwa waenyeji wangu wa jf huku Tanga hawakunipa ushirikiano na mapokezi ya kutosha zawadi iliyo moyoni mwangu narudi nayo Dar es Salaam, shukran za dhati kwa shosti, caramel na michelle kwa mlijitoa kimasomaso kwa karibu ya mdomo japo hamkujua umuhimu wa kampani yenu. Sina budi kuwashukuru kwani hilo si dogo pia.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru The Finest, Kiraka, Baba ubaya, babalao, Miss Judith, Mwenzetu, Babukkijana, MTM, Dreamliner, RayB, Chupaku, Mallaba, Moudymtoi, Miss Pirate, Mpevu, Son of Alaska, na bila kumsahau Shemu, pamoja na wote mliosoma ile post ya "Tanga Mpooooo??? Mmeifanya safari yangu imekuwa ya maana mnenipa kampani ya nguvu sana. Ahsanteni sana tupo pamoja. Walionipa salam zao nimezifikisha na wanasema wamefurahi sana ila watafurahi zaidi kama mtawatembelea siku moja.

Mkuu Ikimita, nimefika Chumbageni kama ulivyoniomba nimemtafuta Rehema nimempata nikampatia ujumbe wako amesema "kapata dereva ajuae gari yake yaenda mbio" sijafahamu ana amamanisha nini lakini sidhani kama atarudi tena kwako. Tanga Raha na ni raha kweli kweli, tanga hakuna foleni kama Dar narudi huku nikifikiria foleni zetu za luku, bank, barabarani na maofisini natamani Dar ingekuwa kama Tanga!

Namalizia kwa kusema naomba mapokezi wandugu ikiwezekana Invisble awe mkuu wa mapokezi na ikibidi kikundi cha matarumbeta kiwepo na si vibaya kama kutakuwa nakikundi cha ngoma za asili especial mdundiko maana huku nilipokelewa na mdumange na waenyeji wangu. Shukran sana na nategemea mapokezi yatafana.
 
karibu tena dar mkuu ni jambo jema kumshukuru mungu kwa kila jambo mkuu ucmaind nilichosema it was joke wala ucninyime zawadi ya halua mkuu kuhusu mapokezi nasubiri ratiba rasmi kutoka kwa mkuu wa kamati ya mapokezi mkuu invisble kama ulivyopendekeza pia ujatumbia unaingia saa ngapi na una2mia air.bus au private nataka niandae red carpet lakukanyagia
 
Shukran sana mkuu na wala sijamind najua utani tu..1ell sasa hivi nipo korogwe nimekuja kuangalia miradi yangu nategemea kuondoka saa sita kuja Dar na usafiri wa Kilimanjaro express Mungu akijaalia salam kwenye milango ya saa kumi nitakuwa Dar InshaAllah.
 
Nipo Korogwe wananchi wanalalamika maji cha ajabu kuna mto unapita katikati ya mji sijui tatizo lipo wapi. Watu wanasema wana wiki sasa maji hayatoki. Poleni sana wanakorogwe kwa madhari nzuri ya kijani kibichi kisha maji yamekuwa kitendawili.
 
waleikhu msalaam, NAOMBA NIWE NI MKUU WA 'ITIFAKI' kwa ajili ya mapokezi yako.
Nadhani barabara zimesafishwa na hautokuta foleni kuanzia kibamba mpaka uingiapo mjini...mafenesi je au sio msimu?
 
waleikhu msalaam, NAOMBA NIWE NI MKUU WA 'ITIFAKI' kwa ajili ya mapokezi yako.
Nadhani barabara zimesafishwa na hautokuta foleni kuanzia kibamba mpaka uingiapo mjini...mafenesi je au sio msimu?

Usijali mkuu nafasi ya ITIFAKI nakuachia wewe, kuhusu mafenesi ninakuja nayo tena first class au unaweza kusema grade A mafenesi ya mnyuzi nyama nyingi kamba kidogo.
 
Nipo Korogwe wananchi wanalalamika maji cha ajabu kuna mto unapita katikati ya mji sijui tatizo lipo wapi. Watu wanasema wana wiki sasa maji hayatoki. Poleni sana wanakorogwe kwa madhari nzuri ya kijani kibichi kisha maji yamekuwa kitendawili.

hili nalo neno...kafa na njaa baharini wakat fish manarukaruka
 
Ukaribiapo tujuze ili vijana wasafishe njia ukiwa bado upo RUVU JUU, maana wananchi watambue kuwa kuna ujio muhimu wa kitaifa.
 
Karibu mpendwa!
Piki piki yangu aina ya Toyo ndio ntakuja nayo. Kwani zinaruhusiwa?
Ndio nipo hapa tegeta nakorofishana nae fundi...tangu ijumaa nlimuachia...nahisi aliitumia week-end nimeiwekea mziki.
Naona ananambia bado inasumbua!
Hata simuelewi...ni muhimu nifike hapo UBT.
 
Ukaribiapo tujuze ili vijana wasafishe njia ukiwa bado upo RUVU JUU, maana wananchi watambue kuwa kuna ujio muhimu wa kitaifa.

Usijali mzee nipo Kabuku nilikaribia nitakujuzeni
 
uFIKAPO rUVU DARAJANI USISAHAU MBOGA-MBOGA, hususan nyanya chungu & mchicha.
Maana mboga za hapa Dar humwagiwa na maji-chafu
 
Ndio mafundi wetu wa kibongo ungeipeleka DT Dibie au Toyota si unajua kama Toyota ni mawakala wa pikipiki za Yamaha Tanzania? Anyway hakikisha airbag zipo maana naogopa sana mzinga wa pikipiki.
 
Shosti naona kimya ndugu hukutaka kunikaribisha kwa vitendo basi hata kuniaga na kunitakia safari njema? Haya yangu mato...
 
Tupo kwatengwe tumesimama na Dereva katuambia ni time ya "kuchimba dawa" haya majani jamani tuking'atwa na nyoka! Hivi Serikali kwanini isijenge vyoo mfano wa kile cha view point ya lake manyara kwa ajili ya wasafiri?
 
Ndio mafundi wetu wa kibongo ungeipeleka DT Dibie au Toyota si unajua kama Toyota ni mawakala wa pikipiki za Yamaha Tanzania? Anyway hakikisha airbag zipo maana naogopa sana mzinga wa pikipiki.

tumuombee huyo fundi asizidi kumweka kwenye foleni....maana nahisi huyo fundi hana nia njema.
 
Tupo kwatengwe tumesimama na Dereva katuambia ni time ya "kuchimba dawa" haya majani jamani tuking'atwa na nyoka! Hivi Serikali kwanini isijenge vyoo mfano wa kile cha view point ya lake manyara kwa ajili ya wasafiri?

tatizo lako ukufatilia kampeni vzuri yote yapo kwenye ahadi za JK kujenga vyoo hivyo maeneo yote hayo ya kuchimbia dawa
 
mkuu karibu da hio laptop yako ina nguvu sana naona unaitumia tangu morning na bado iko ngangari
 
ukifika pale chalinze uninunulie korosho na chanuo!
Nimeamua ni kodishe boda boda...siunajua tena foleni kuanzia hapa mawasiliano hadi ubungu inasumbua jioni.
 
mkuu karibu da hio laptop yako ina nguvu sana naona unaitumia tangu morning na bado iko ngangari

Nina laptop Dell studio lakini siitumii natumia BlackBerry 9700 Bold ndio maana nawawezesha kujua yanayojiri safarini. Anyway ninakaribia vigwaza sijui nimeandaliwa njia gani kuelekea ChangKombe ambayo haina jam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…