Dar es Salaam here I come naomba mnipokee waugwana!

Dar es Salaam here I come naomba mnipokee waugwana!

ukifika pale chalinze uninunulie korosho na chanuo!
Nimeamua ni kodishe boda boda...siunajua tena foleni kuanzia hapa mawasiliano hadi ubungu inasumbua jioni.

Maalim Noamba nitabirie ila mambo mazuri tu
 
Huna lolote wewe,nimekupa number kupiga pia umeona ntafaidi haya bwana.

Namba uliyonipa nikipiga inaniambia haijapewa mteja "tafadhali iangalie vizuri kisha upige tena" nadhani digit moja ulisahau kuiiandika!
 
Nimependa sana jinsi ulivyo pangilia mawazo yako hakika kushukuru ni jambo jema.
Asalam alaikum wanajamvi, Namshukuru Mungu kwa kuiona siku mpya nikiwa na siha na afya njema. Baada ya kufika Tanga kuwaona jamaa na marafiki na sio kurenuu konsensa kama alivyosema "drphone" hatimae leo nipo njia moja narudi zangu Dar es Salaam.

Nimefungashiwa na wenyeji wangu pakacha la embe viringe, nazi, ndizi za bokoboko,halwa, vitoria,heltho ya lita 5 na vingine vingi. Japo kuwa waenyeji wangu wa jf huku Tanga hawakunipa ushirikiano na mapokezi ya kutosha zawadi iliyo moyoni mwangu narudi nayo Dar es Salaam, shukran za dhati kwa shosti, caramel na michelle kwa mlijitoa kimasomaso kwa karibu ya mdomo japo hamkujua umuhimu wa kampani yenu. Sina budi kuwashukuru kwani hilo si dogo pia.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru The Finest, Kiraka, Baba ubaya, babalao, Miss Judith, Mwenzetu, Babukkijana, MTM, Dreamliner, RayB, Chupaku, Mallaba, Moudymtoi, Miss Pirate, Mpevu, Son of Alaska, na bila kumsahau Shemu, pamoja na wote mliosoma ile post ya "Tanga Mpooooo??? Mmeifanya safari yangu imekuwa ya maana mnenipa kampani ya nguvu sana. Ahsanteni sana tupo pamoja. Walionipa salam zao nimezifikisha na wanasema wamefurahi sana ila watafurahi zaidi kama mtawatembelea siku moja.

Mkuu Ikimita, nimefika Chumbageni kama ulivyoniomba nimemtafuta Rehema nimempata nikampatia ujumbe wako amesema "kapata dereva ajuae gari yake yaenda mbio" sijafahamu ana amamanisha nini lakini sidhani kama atarudi tena kwako. Tanga Raha na ni raha kweli kweli, tanga hakuna foleni kama Dar narudi huku nikifikiria foleni zetu za luku, bank, barabarani na maofisini natamani Dar ingekuwa kama Tanga!

Namalizia kwa kusema naomba mapokezi wandugu ikiwezekana Invisble awe mkuu wa mapokezi na ikibidi kikundi cha matarumbeta kiwepo na si vibaya kama kutakuwa nakikundi cha ngoma za asili especial mdundiko maana huku nilipokelewa na mdumange na waenyeji wangu. Shukran sana na nategemea mapokezi yatafana.
 
Hilo nalo neno...)Aani nilivyochoka natamani ningekaribishwa na kungekuwa na members wakike walioteuliwa makhsusi kwa ajili ya kunifanyia massage.

Kwani akiwa wakiume kutakua tatizo?
Yupo jamaa yangu wa kiume anaiweza hiyo kazi ya massage!
Nipe namba zako nimpe muwasiliane nae! Au nikupe namba zake?
 
Kwani akiwa wakiume kutakua tatizo?
Yupo jamaa yangu wa kiume anaiweza hiyo kazi ya massage!
Nipe namba zako nimpe muwasiliane nae! Au nikupe namba zake?
Hili nalo nenooo,toa namba kaka upate massage:laugh:
 
Kwani akiwa wakiume kutakua tatizo?
Yupo jamaa yangu wa kiume anaiweza hiyo kazi ya massage!
Nipe namba zako nimpe muwasiliane nae! Au nikupe namba zake?

Napenda mwili wangu uguswe na jinsia tofauti na mie maana kwenye massage sometimes kunakuwa na mitekenyo na ndio maana hata wakina dada "wanasuguliwa" miguu na kina kaka kuna siku nimekuta mwanamke pale CBE pub anasuguliwa miguu anatekenyeka mpaka raha sijui kama hajaji....................
 
Hili nalo nenooo,toa namba kaka upate massage:laugh:

Hapo itakuwa ngumu sana shosti ukizingatia mikono ya kiume ina sugu badala ya kupata relaxation na sensation nitapata mikwaruzo ya sugu.
 
Ukifika majani mapana,kabla ya mizani,angalia kulia kuna nyumba yangu ndogo inajengwa,iangalie vizuri kisha ulete ripoti naona mafundi wananchanganya. Utaiöna inajengwa kwa tofali nyeusi,usisahau.
 
Hapo itakuwa ngumu sana shosti ukizingatia mikono ya kiume ina sugu badala ya kupata relaxation na sensation nitapata mikwaruzo ya sugu.

Hahahahahahaaaa,sio yote kuna mingine lainiiiiiii,acha woga toa namba hiyo ukatolewe uchovu wa safari.
 
Baada ya hapo usisihau kupita kijijini kwetu
Karibu sana
 
Back
Top Bottom