Naangalia kipindi cha Sports AM kinachorushwa na Azam Sports 1,
anahojiwa Rais wa TFF Karia kuhusiana na kuchelewa kufunguliwa mageti ya
uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo watu ni wengi sana na wapo nje kiasi
amani inaanza kuvurugika.
Rais anajibu kwamba yeye hausiki na suala hilo na lipo chini ya maafisa wa
CAF na afisa wa TFF anayeshirikiana nao watu wa CAF, kwa hiyo yeye hajui chochote
walichokubaliana wala walichopanga.
Majibu haya kwa mtu anayesimamia chombo cha mpira si sahihi. Hata kama yeye hayupo
kwenye hiyo kamati ya usimamizi anawajibu wa kujua walichopanga, hata kushauri.
Kwamba unaona kabisa kuna hali ya mvurugiko nawe kama kiongozi wa Mpira unasema huusiki.
Kwa hiyo unasubiri mambo yaharibike kisha zigo wapewe wengine.
Tanzania imetia nia ya kuandaa michuano ya mataifa ya Afrika, sasa kama mechi ya fainali
Rais anajitoa na wala haoneshi kutaka kutatua tatizo kweli tunaweza kupewa hiyo nafasi?
Viongozi wetu hupenda kujiweka mbele kwenye mafanikio hata kama sio yao, lakini
panapotokea changamoto wajifanya kutohusika.