Dar es Salaam: Mfumo wa uzoaji taka mitaani unaweza kusababisha athari za kiafya kwa Wananchi

Dar es Salaam: Mfumo wa uzoaji taka mitaani unaweza kusababisha athari za kiafya kwa Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakati Mikoa kadhaa ikiripotiwa kuwa na mlipuko wa Kipindupindu na Magonjwa ya Tumbo ikiwemo Mwanza, Shinyanga na Simiyu, upande wa Mitaa mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam ina changamoto ya kukosekana mfumo mzuri wa utunzaji na uzoaji kutoka kwenye makazi ya Watu na sehemu za biashara.

Baadhi ya mitaa iliyopo karibu na Barabara Kuu, makazi ya watu na sehemu za biashara kuna taka zimekusanywa kwa siku kadhaa bila kuchukuliwa na Mamlaka zinazokusanya kwa ajili ya kwenda kuzipeleka kwenye Dampo hali inayohatarisha afya.
Mwenge Kituo cha Daladala.jpg

Mwenge Kituo cha Daladala
Mwenge Kwa Muuza Juisi.jpg

Mwenge Madukani
Tabata Dampo (Kituo cha Daladala) (1).jpg

Tabata Dambo Kituo cha Daladala
Morocco Darajani.jpg

Morocco Kinondoni (chini ya Daraja)​
 
Waingie sinza na tandale ndani ndani huko watakutana na njia nzuri za kutunza na kusambaza kipindupindu
 
Kila Halmashauri ijitahidi iwe na dampo lake..PUGU ni mbali,hivyo huongeza gharama za uendeshaji kwa Wakandarasi

Lakini pia Elimu ya kutenganisha taka nyumbani itolewe ili taka mali zibaki kwa matumizi mengine

Bado Private haijashirikishwa vya kutosha,pia Serikali iweke MAZINGIRA mazuri ya uwekezaji,kama MIKOPO na UDHAMINi kwa wakandara wadogo

Yote kwa yote TAKA ni MALI
 
Back
Top Bottom