TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Waafrika tuna dharau sana hasa viongozi walioshika mpini.
Mwaka fulani hapa jijini Dasalam kuna project flani ililetwa nadhani na UN kuhusu kuboresha miundombinu ya jiji na bahati flani niliwahi kuwepo as mdau wa taasisi flani.
Kutokana na karabrasha nililonalo lenye michoro yote ya jiji la Dasalam, kwa kiasi kikubwa wale watoa pesa walizunguka karibu mji wote na kurudhishwa na maboresho hayo ila nachekea kuandika, walikata tamaa, mfano kuna kitu waelewa mnakiona pale manzese Tiptop ile barabara ilivyo.
Magomeni kanisani kuja hadi Mkwajuni eneo hilo ilikuwa paboreshwe, jangwani ilikuwa pajengwe tourism area maji yaachwe yajae lakini ktk mfumo ambao pasingekuwa na mafuriko.
Bahati mbaya kabrasha langu limesombwa na maji laiti lingekuwepo ningewawekea hata picha hapa, but endapo nitalipata maji yakituwama tutapata kile ninacho maanisha.
Baadhi ya vongozi wa kiafrika hawana mipango imara na endelevu kwa nchi zao, wanasukuma gurudumu kwa mambo yanayoifanya nchi iende but not long term issues kama nchi za wale waliofunguka akili huko ulaya.
Badala ya kuendeleza majukwaa ya kusulubishana kisiasa nilidhani nguvu hizo zingeweza kutumika kufanya mapinduzi katika kuwawekea raia wa kawaida mazingira rafiki, iwepo mvua au jua basin raia aendelee na majukumu yake ya kuutafuta mkate wake wa siku.
Si kila raia anauwezo wa kutunza kwenye kibubu shs anayochuma kila uchao, asilimia kadhaa ni kula kwake kunategemea na mguu wake.
Watoto, wajukuu wajao watakuja kuyachapa makaburi yetu bakora kutokana na udhaifu mkubwa wa kimfumo tunaowaachia.