kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Unaushahidi na kauli ile kule Zanzibar umeshasahau eti eeeTISS wanasema michezo hii wameacha kufanya
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaushahidi na kauli ile kule Zanzibar umeshasahau eti eeeTISS wanasema michezo hii wameacha kufanya
Tuhame geto eti au unataka kutushaur nnApumzike kwa amani
Jamani hakuna kitu naogopa kama kufa na hamna mtu karibu. Aisee vijana swala la kuishi getto peke yako sio vizuri. Unaweza ukapata shida hamna wa kukusaidia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna funzo kubwa sana hapa ktk andiko lako,ubarikiwe sana japo jina lako linanipa hofu na mashaka sana mkuu.Depression is real. Ukimuona mtu mwenye matatizo mpe pole, mfariji, mkumbatie, mwambie unampenda, onesha nia ya kumsaidia hata kama iko nje ya uwezo wako just muoneshe njia sahihi tu basi. Maana wengine wanatembea nyuso zikitabasamu huku mioyo yao ikilia kilio kikuu.
mizinga mingiMambo ya kupanga chumba halafu unaishi mwenye shida zake ndo hizi bora ukae hata na ndugu au hata manzi atakusaidia siku ya madhila kama haya
Usomapo uwe makini, mbona alipokuwa anafanyia kazi kwa mara ya mwisho pametajwa? Ulitaka mpaka waseme BBC,CNN au Aljazeera, ndiyo ungeelewa?Cha kushangaza hiyo habari imeandikwa na mwandishi wa habari!
Ukifa, umekufa, haijalishi umekufa wima au umesimama!Mambo ya kupanga chumba halafu unaishi mwenye shida zake ndo hizi bora ukae hata na ndugu au hata manzi atakusaidia siku ya madhila kama haya
WasuKUMA wasipewe urais tena.Dar es Salaam. Mwandishi wa habari Deogratius David amekutwa amekufa chumbani kwake Buguruni jijini Dar es Salaam baada ya kutoonekana kwa siku kadhaa.
Mwili wake umekutwa katika chumba hicho leo Jumatatu Januari 27, 2020 baada ya majirani kuanza kusikia harufu kali.
Mwananchi lilifika eneo hilo na kuzungumza na majirani waliosimulia jinsi polisi walivyofika na kuuchukua mwili wa mwandishi huyo wa habari.
Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu taarifa za kifo hicho kamanda wa polisi Wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela amesema hana taarifa zozote.
Kwa sharti la kutotajwa jina mmoja wa majirani amesema, “Deo hajaonekana kwa siku kadhaa na kwenye simu hapatikani lakini kilichotupa wasiwasi ni harufu kali iliyokuwa inatoka kwenye chumba chake.”
“Asubuhi ya leo tukavunja mlango ndio alipokutwa akiwa kitandani kwake mwili ukiwa umeharibika vibaya, hilo ndilo linaloweza kusema kwa kifupi mengine watakuwa nayo polisi.”
Habari zaidi zinaeleza majirani walitoa taarifa polisi waliofika eneo hilo na kuchukua mwili wa mwandishi huyo.
======
TANZIA TANZIA TANZIA
TAARIFA RASMI KUHUSU KUFARIKI KWA MWANDISHI WA HABARI DEOUGLAS DAVID
Leo tarehe 27/1/2020 tumepokea taarifa ya msiba wa mwandishi wa habari ndugu yetu Deouglas David ambaye kifo chake kimemkuta nyumbani kwake eneo la Buguruni jijini Dar es salaam,
Deouglas amekutwa amefariki chumbani kwake eneo la Buguruni baada ya majirani zake kuanza kuhisi harufu kutoka chumbani kwake ndio wakafanya utaratibu wa kufungua mlango kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ya mtaa chini ya usimamizi wa jeshi la polisi kituo Polisi Buguruni,Walipofungua Mlango walimkuta ndugu Deouglas David amelala kitandani huku akiwa amefariki kwa takribani siku tano
. Baada ya hapo polisi kwa kushirikiana na ndugu zake pamoja na baadhi ya waandishi wamempeleka Hospital ya taifa ya Muhimbi.Kwa taarifa za awali inasemekana ndugu Deoglas alikuwa na matatizo ya Kudondoka (Kifafa).baada ya kuwasiliana na mzazi wake aliyeko Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa ameomba sisi waandishi,marafiki na ndugu zake wa karibu tusaidie kumsafirisha ndugu yetu Deoglas kwenda nyumbani Sumbawanga kwa ajili ya mazishi.
Hivyo basi kwa taarifa hii tunaomba waandishi wa habari,marafiki,na ndugu na watu wote wakiwemo wadau wa habari kuungana nasi katika kipindi hiki Cha Msiba huu mzito wa mwanahabari mwenzetu ndugu Deoglas David . Utaratibu wa kumsafirisha mwenzetu Deoglas unaratibiwa na marafiki pamoja na ndugu zake walioko jijini Dar es salaam na tunategemea kusafirisha mwili wa marehemu kesho tarehe 28/1/2020 kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa .Hivyo tunaleta kwenu wadau wa habari wote ambao wataguswa na Msiba huu kuweza kutusaidia kumhifadhi mwenzetu Deoglas katika makazi yake ya milele.
Katika enzi za uhai wake Deoglas David aliwahi kufanya kazi katika Vyombo vya habari vya DARMPYA BLOG&TV ONLINE, LEMUTUZ BLOG&TV ONLINE na hatimaye mpaka kifo kinamkuta alikuwa anafanya kazi kwa kujitolea katika kituo Cha TBCONLINE
Kwa taarifa zaidi wasiliana na
John Marwa(Mkrugenzi Darmpya blog & TV Online)
0763047070
Kamati ya Kuratibu msiba wa Deoglas David inaongozwa na
1.Benard Mwakyembe ,Diwani wa kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke 0712393938
2.John Marwa(Mkurugenzi&Mwendeshaji DARMPYA BLOG &TV ONLINE 0763047070
3.Brigiter Masaki (Mwandishi wa Mtanzania 0712915944)
4.Hamis Holela (TBCONLINE 0787393639)
5.Maria Kalonga(LEMUTUZ ONLINE 0653020521)
Tunapokea michango yote kupitia kamati hii ya uratibu ,namba ya kutuma michango ni
0763047070 M: PESA (ONETIME LIMITED)
Kwa kweli unaajiriwa na mtu kama LEMUTUZ kwa nini usife mapemaMaisha tunayoishi ni stress,
Vyakula tunavyokula ni stress,
Waajiri nao ni stress!!
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu una uhakika na hicho unachokisema!? au kuhusisha na TISS?! naona kwenye habari hapo imeandikwa alikua na kifafa, letc say "alikua ndani kikamshika ,kwakua hakukua na huduma ya kwanza akaanguka hali ya kua kang'ata ulimi kitu kilichopelekea akapata suffocation". umezingatia possibility kama hii!?.TISS wanasema michezo hii wameacha kufanya
Yaani mwajiriwa wake amekaa siku zote bila mtu kuripoti kazini hata kutoa taarifa hamna au alikuwa likizo?
Afadhali walivyokuwa wanawapa kesi za uhujumu, afadhali walivyokuwa *wanawateka na kuwapa kesi* kuliko hii *staili*.